Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, ametembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi katika jengo la Kituo cha Polisi cha Kata ya Masasi, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.
Jengo hilo limejengwa na Bw. Iman Haule kupitia KUAMBIANA INVESTMENT COMPANY LIMITED ikiwa ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya usalama na kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi.
Mhe. Naibu Waziri Mahundi amepongeza hatua hiyo, akieleza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya usalama unachangia kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao, kuongeza upatikanaji wa haki na kuleta mazingira wezeshi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.











Post A Comment: