Na Denis Chambi, Tanga .

JUMUIYA YA  Afrika Mashariki (EAC) umezipongeza nchi za Tanzania na Kenya kwa kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa forodha ambao umeweza kuchangia ongezeko la ukusanyaji wa kodi kupitia mamlaka zake za Tanzania Revenue Authority 'TRA' na Kenya Revenue Authority 'KRA' pamoja na kuboresha miundombinu inayotumika.

Hatua hiyo pia  imeweza kuwapa uelewa mpana na kuwasaidia  wafanyabiashara  hususani wajasiramali wadogowadogo waliopo katika nchi hizo kujua umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati pamoja na kuwapa fursa ya kuuza bidhaa zao ndani ya Afrika Mashariki hatua ambayo imewawezesha kukuza mitaji yao.

Akitoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea  kituo cha  Horohoro kwa upande wa Tanzania na kile cha  Lungalunga kwa upande wa Kenya Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya Afrika ya  Mashariki (EAC) Annet Semwamba amesema kuwa malengo ya kuanzishwa kwa umoja huo yameendelea kukua katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara  huku wakiendelea kutatua  changamoto nyingine  zilizopo ambazo bado zimeendelea kuwa kikwazo baina ya nchi wanachama




"Tumefurahi sana kuona kwamba mapato yameongezeka kwa upande wa TRA na KRA ambapo pesa mnazokusanya zinakwenda moja kwa moja katika kuboresha na kutoa huduma za kijamii na hivyo kugusa maisha ya wananchi wa hali ya chini tunaona barabara zimejengwa , hospitali,  elimu na kadharika" amesema Semwamba.


"Lakini pia tumefurahi kuona kuwa miundombinu ambayo ipo inatumika ipasavyo kwa sababu yapo baadhi ya maeneo ipo miundombinu kama hii lakini haitumiki kama vile ambacho inatakiwa" ameongeza.


Moja wapo ya malengo ya pango wa Umoja wa Afrika 'EAC' ni kuhakikisha  kuwa nchi zote nane  zilizopo ndani ya Umoja huo zinatumia sarafu moja  ili kuwawezesha na kuwasaidia wafanyabishara kupata urahisi wa kuuza na kuzitangaza biashara zao ndani na nje. 


Semwamba amezitaka nchi zote wananchama kupitia wimbo wa Afrika Mashariki kuuishi kwa vitendo kupitia tungo na maneno yaliyotumika  hatua ambayo itawezesha kufikia malengo ya kuanzishwa kwa Umoja huo.

Awali akizungumza  Afisa mfawidhi kutoka katika kituo Cha Horohoro Shadrack Mbona ameeleza  kuwa  kumekuwa na mafanikio  yaliyochangiwa na ushirikiano baina ya vituo hivyo ambapo kwa upande wa Tanzania kupitia kituo cha Horohoro ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 306 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi Bilioni 548  kwa mwaka 2024/2025.


"Ufanyaji wa biashara umekuwa ukikuwa mwaka hadi mwaka  kwa mfano kwa mwaka wa fedha 2022/2023 sisi kama kituo cha Horohoro tuliweza  kukusanya Bilioni 306 mwaka unaofuata imeenda adi Bilioni 408 mwaka unaofuata imeenda hadi Bilioni 548 kuna ongezezo la Bilioni 100 kila mwaka  na hii jnawezekana kwa sababu tunaboresha huduma" amesema.


Aisha Mbonea ameoeleza kuwepo kwa   utaratibu wa kutoa elimu kwa wafanyabiahara wadogowadogo  kuhusu jinsi ya kuwasaidia kuhusu taratibu za kufuata wakati anapohitaji huduma ya kwenda kuuza ama kununua bidhaa kwa upande wa Tanzania na Kenya.


"Tumekuwa na utaratibu wa kupitia kwenye masoko yaliyopo mipakani kwetu na kutoa elimu kwa wafanyabiahara  kuhusu hatua ambazo wanatakiwa kuzifuata na sasa Wana uelewa wa kutosha na imekuwa na mafanikio makuba sana na sisi tutaendelea na utaratibu huu" amesema


Amesema kuwa badokatika kituo hicho  kuna uhitaji mkubwa wa matumizi ya kifaa ya kisasa ya utambuzi wa mizigo 'Scanner machine' kwaajili ya kutambua na kubaini bidhaa ambazo zinapitushwa na wafanyabishara wa  nchi zote mbili.


"Maendeleo haya yanahitsji vituo vya kisasa zaidi kwa sababu  mahitaji yanaongezeka  kuna mizigo mingi ambayo  kwa kukagua moja moja unaweza kutumia muda mrefu hivyo kumekuwa na changamoto ya ukaguzi ambayo inahitaji sasa kuwepo kwa matumizi ya Scanner ili kupunguza muda wa ukaguzi na kuimarisha ulinzi na tutahakikisha usalama wa nchi zote mbili" amesema Mbonea.

Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: