Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Baraza la Taifala Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC) wakati alipofanya ziara MakaoMakuu ya NEMC, Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Julai 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira (NEMC), kufanya kazi kwa bidii, weledi, ushirikiano nakujiepusha na vitendo vya rushwa ili kuifanya Taasisi hiyo kuwa chachu yauhifadhi wa mazingira na maendeleo ya Taifa.
Makamu wa Rais ametoa wito huo, alipofanya ziara Baraza la Taifa la Hifadhina Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Makao Makuu, Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Amewataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kutokuwakikwazo katika utekelezaji wa miradi mikubwa kwa kutanguliza maslahi yaTaifa mbele.
Makamu wa Rais ameipongeza NEMC kwa kutimiza miaka 40 tangukuanzishwa kwake na kuendelea kuwa chombo kinachohitajika nakutumainiwa nchini.
Aidha, Makamu wa Rais ameipongeza NEMC kwa Mpango Mkakati wa miakaMitano ambao umeanisha vitu mbalimbali vitakavyowezesha usimamizi nautunzanji wa mazingira kwa ufanisi.
Amesema uanzishwaji wa mashindano yauhifadhi wa mazingira ni muhimu kwa kuwa itakua hamasa ya upandaji mitina usafi kitaifa.
Vilevile, Makamu wa Rais amesema ili kudhibiti masuala ya uchafu ni vema pia kuwatambua wanaokuwa wamefanya vibaya katika mashindano ya usafi nakuwataja hadharani ikiwemo kupatiwa vyeti.
Ameiagiza Ofisi ya Makamu waRais, Muungano na Mazingira, kushirikiana na NEMC katika kufanikishamashindano ya usafi na utunzaji mazingira nchini.
Halikadhalika Makamu wa Rais, ameitaka NEMC kutilia mkazo suala la nishatisafi, matumizi ya teknolojia za kisasa katika kulinda mazingira pamoja nakusimamia vema suala la urejerezaji taka.
Makamu wa Rais, amewapongeza Viongozi wa NEMC kwa kuendelea namchakato wa kuifanya NEMC kuwa Mamlaka kamili. Amesema suala hilolinashughulikiwa na katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita limepewaumuhimu wa kipekee.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Emmaculate Sware amesema NEMC imeaandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano yaani mwaka 2026/2027 – 2030/2031 ambao umelenga kuongeza ufanisi wa usimamizi wa mazingira, kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali, kuimarisha ukaguzi nautekelezaji wa sheria pamoja na kuchochea uchumi wa kijani na ustahimilivuwa mabadiliko ya tabianchi.
Ziara hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Masauni pamoja na Katibu Mkuu Ofisiya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Emmaculate Swaremara baada ya kuzungumza na Viongozi na Watumishi wa Baraza hilo,alipofanya ziara Makao Makuu ya NEMC, Mikocheni Jijini Dar es Salaam leotarehe 02 Julai 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu waBaraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. EmmaculateSware pamoja na Watumishi waliofanya kazi pamoja na Makamu wa Raiswakati akifanya kazi Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC). Picha hiyo imepigwa mara baada ya Makamu wa Rais kukamilishaziara aliyoifanya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mikocheni Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 02 Julai 2026. 







Post A Comment: