Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, amevutiwa na mfumo wa Kupanga na Kusimamia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). 

Mhe. Kikwete ameipongeza REA kwa kuja na mfumo huo mara baada ya kutembelea banda hilo kwenye ufunguzi wa Maadhimiaho ya Wiki ya Utumishi kwa Umma 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. 

Mfumo huo (*REA DIGITAL PLATFORM*) unaonyesha miradi yote inayotekelezwa na REA na kuweza kuisimamia kidijitali na kuwapa taarifa wadau popote walipo duniani kuhusiana na miradi ya Nishati vijijini.

Akimueleza Mhe. Kikwete, Afisa Upimaji Mwandamizi wa REA, Bw. Hussein Shamdas ameeleza kuwa kupitia mfumo huo mwananchi anaweza kujua mipango ya Wakala kwenye eneo lake na kufuatilia miradi inayotekelezwa na Wakala katika eneo husika.
Share To:

Post A Comment: