Na; Mwandishi Wetu - Chato

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Mohammed Ali Sheikh, Ametoa wito kwa wataalam kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu kuwa na mbinu bora za kiutendaji zitakazowezesha programu hiyo kutekelezeka kwa kasi zaidi.

Ameyasema hayo Wilayani Chato Mkoani Geita Tarehe 12 Juni 2026 alipozungumza na wataalam wa programu wanaofanya kazi ya utekelezaji ya mapitio ya programu mara baada ya ziara yake maalum ya kutembelea kituo cha kuendeleza Ukuzaji viumbemaji cha Rubambagwe kilichopo Wilayani chato.

“Niwapongeze sana kwa kuchukua hatua za haraka baada na maagizo ya kikao cha Mawaziri kukaa pamoja kama wataaalamu na kuyafanyia kazi maagizo yale. Hii ni hatua muhimu sana inayoonesha ni kwa namna gani mnaweza kuwajibika kiutaalamu, mnapewa maelekezo na mnayatekeleza” Alisema.

Naibu Katibu Mkuu Sheikh alibainisha kuwa, kukutana kwa wataalamu hao ni hatua muhimu sana ya kukaa pamoja na kujaribu kujitathmini kuona kila kinachofanyika kinakwenda sawa ama vinginevyo, ‘’Niipongeze sana timu ya Uratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuitisha kikao kazi hiki “Mnapoona kitu hakiendi hebu muitane muone namna ya kukifanyia kazi sisi kama watekelezaji wa Programu hii ni familia moja, Serikali ni moja na tunachotaka ni kufikia malengo na kumsaidia mtanzania katika kilimo na uvuvi kwa ukubwa wake” Alisisitiza

Alibainisha kuwa, kwa kufanya tathmini kunasaidia kujua wapi ulikwama na wapi pa kuboresha. Zaidi aliendelea alisema kuwa, kukua na kubadilika kwa teknolojia kufanya tathmini kunaweza kusaidia kwenda mbele zaidi, “lazima tusaidianae tuje na mbinu bora za utekelezaji katika utendaji wa mradi msione aibu kushauri na kutoa mapendekezo ya kiutendaji kuhusiana na Programu.” Alisema

Akizungumza katika kikao kazi hicho, Mhandisi Enock Nyanda, Mkurugenzi msaidizi sehemu ya Sekta za Uchumi na Uzalishaji Idara ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) alisema lengo mahususi ya wataalam kukutana katika kikao kazi hicho ni kuongeza kasi ya utekelezaji wa Programu ili kufikia malengo.
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: