Kwa miaka mitatu, maisha yangu yalizunguka jambo moja tu. Kutafuta kazi. Kila asubuhi niliamka nikiwa na matumaini mapya. 

Nilifungua simu yangu na kutafuta matangazo ya kazi, nikatuma maombi, na kusubiri majibu ambayo mara nyingi hayakuwahi kufika.

Mwanzoni nilikuwa na matumaini makubwa.

Nilijiamini kuwa elimu yangu na uzoefu wangu vingekuwa vya kutosha kunisaidia kupata nafasi nzuri. Lakini kadri muda ulivyopita, nilianza kuona hali ikiwa tofauti na nilivyotarajia.
Miezi iligeuka miaka.

Nilituma maombi kwa kampuni nyingi sana. Wakati mwingine niliitwa kwa mahojiano lakini sikuchaguliwa. Mara nyingi sikupata hata majibu ya maombi niliyotuma. 

Kwa kweli hali ile ilinivunja moyo. Kilichoniumiza zaidi ni kuona marafiki zangu wakipata kazi na kuendelea na maisha yao huku mimi nikiendelea kusubiri nafasi yangu.

Nilianza kujiuliza kama kulikuwa na kitu nilichokuwa nakosea. Kadri miaka ilivyopita, confidence yangu ilianza kupungua. 

Kulikuwa na nyakati nilitaka kuacha kutuma maombi kabisa. Nilihisi kama kila juhudi niliyokuwa nikifanya hazikuwa na matokeo yoyote. Lakini sikuwa tayari kukata tamaa. SOMA ZAIDI.

Share To:

Post A Comment: