Na Oscar Assenga, TANGA
BODI ya Wakurugenzi ya Bonde la Pangani leo wamefanya ziara ya kukagua maeneo vyanzo vya maji ikiwemo Bwawa la Mabayani na Mtambo wa Kutibu Maji wa Mowe na kujiridhisha kuhusiana na kazi zinazotelezwa na menejimenti pamoja na wateja wao namna wanavyopokea huduma.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bonde la Pangani,Mhandisi Ruth Koya alisema kwamba bodi hiyo na menejimenti wamefanya ziara hiyo kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa maelekezo na majukumu wanayowalekeza menejimenti kwamba wanayafuatilia na kuyafanya kwa uhakika.
Katika ziara hiyo Bodi hiyo wametembelea Bwawa la mabayani wamejionea shughuli Zinazofanyika ikiwemo utunzwaji wa Bwawa la mabayani pamoja na kumtembelea mteja wao mkubwa Tanga Uwasa wameona yupo vizuri na kazi inafanyika kwa waledi
Alisema kwamba wameona bwawa limewekwa alama na wameipokea taarifa kwamba wananchi nao wanashirikishwa kutokana na uwepo wa jumuiya za watumia maji ambao wamekuwa chachu kubwa kuhakikisha vyanzo hivyo vinalindwa na kutunzwa.
Aidha alitoa wito kwa watumishi na kusisitiza kuwasimamia wadau wao wakiwemo Tanga Uwasa ili kuendelea kutunza chanzo cha maji kikubwa ambacho ni muhimu kwa ajili ya Jiji la Tanga na kushirikiana na wadau Tanga Uwasa na wengineo .
Alisema kwamba lakini wamepata taarifa Tanga Uwasa wanazidi kupanua uzalishaji maji hadi kufikia lita milioni 70 ina maana utunzaji ni nzuri ndio maana wameweza kuwekeza zaidi kupitia hat fungani yao walioipata hivi karibuni.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Bonde la Pangani Segule segule alisema kwamba ziara ya Bodi hiyo ni kutembelea maeneo ya uwandani na kukakgua maeneneo mbalimbali na kujiridhisha kuhusiana na kazi zinazotekelzwa na menejimenti lakini kupata kujua kuhusu wateja wao mbalimbali wanavyopokea huduma zao.
Alisema kwamba bodi imeona ipite kwenye eneo la mnufaika mkubwa wa maji Mto Zigi ambao ni wenzao wa Tanga Uwasa ambapo wametembelea maeneo mbalimbali ambayo Tanga Uwasa wanafaidika nayo wamenza ikiwemo Bwawa la Mabayani ambalo wao ndio wamiliki na yeye ndio mteja wao.
Aidha alisema kwamba wamejionea mazingira yanavyotunzwa na wametumia fursa hiyo kupata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa kuhusiana na mradi wa Hati Funfani ambao unatumia chanzo kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji Tanga .
Alieleza kwamba na ziara ilitoa fursa kwa wajumbe wa bodi,menejimenti kuona mchango wao kama bonde mchango wao kwenye mradi Hatifungani kwamba wakitunza vyanzo vyema wenzao wa Tanga Uwasa wataweza fikia matarajio yao na kwa gharama walizokadiria.
Aliongeza kwamba bwawa hilo wanalitunza na moja walishaanza kuweka alama za mipaka kuainisha mita 500 na kama sheria za usimamizi rasilimali za maji zinaelekeza mita 60 za chanzo lakini wanatoa mamlaka kwa taasisi na wao kama mabonde kuomba nyongeza kwa bwawa la mabayani wamehifadhi mita 500 .
Alieleza kwa sasa hiyo inatoa fursa hata nyongeza za miradi kutokana na mahitaji ya maji wanaweza kuhifadhi hivyo mkakakati wao ni kuendelea kuimraisha baada ya kuweka alama za mipaka katika yale maeneo walioweka mipaka watu wasifanye shughuli za kibinadamu ili kupunguza uchafuzi kwenda kwenye bwawa.
Aliongeza kwamba lakini upande wa juu wa bwawa wanaendelea kuimarisha utunzaji wa jumuiya za watumiaji maji ambao wote wanakuwa watumiaji maji na mkakati wa kuziimarisha huku wenzao Tanga Uwasa wameimarisha utunzaji wa vyanzo vya maji .
Hata hivyo alisema kwamb hali ya vyanzo vya maji ukilinganisha na miaka ya nyuma ni nzuri changamoto zipo lakini hawajafika wakati wa kusema hali iliyopo imehataraisha vyanzo kukauka na kushindwa kuwahudumua watu.
Aliongeza kwamba lazima waendelee kuimarisha na shughuli zinaongezeka kutokana na mahitaji ya ardhi kuna jitihada kubwa za watu kutokana na uhaba wa ardhi na watu wanaongezeka na kutaka kusogelea vyanzo wao wanaendelea kuimarisha jumuiya za watumiaji maji ili kuweza kuhakikisha vyanzo vya maji vilivyopo vinatunzwa na kuvilindwa.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema kwamba ameshiriki katika ziara hiyo ya Bodi ya Bonde la Pangani ambao wanatembelea kuangalia vyanzo vya maji vinavyotunzwa ikiwemo bwawa la mabayani ambalo ndio chanzo kikubwa wanachotumia Tanga Uwasa katika kusambaza maji kinahudumia Tanga, Muheza na Mkinga .
Mhandisi Hilly alisema wameongeza uzalishaji wa maji kuhakikisha wanawafikia vema wananchi ili kutekeleza malengo yao mbalimbali ya nchi ifikapo 2030 watu wote wawe wamepata maji mijini na Tanga Uwasa na wenzao Ruwasa wananchi waweze kupata maji.
Alisema kwa hiyo mahitaji na matumizi ni makubwa wao kwa kushirikiana na Bodi la Bonde la Mto Pangani wanaweka juhudi kubwa katika utunzaji chanzo cha maji kutokana na kuwa wanufaika wakubwa wa bonde hilo.
Alieleza hivyo wana wajibu kuhakikisha chanzo hicho kinalindwa na kutunzwa wanashirikiana kwenye maeneo mbalimbali ya mto,bwawa la mabayani wana mpaka kamati za uhifadhi na utunzaji wa mazingira ikiwemo uwamakizi kuhakikisha vinaendelea kuwa imara.
“Kwa mfano mradi wa hati fungani miongoni mwa fedha zinakwenda kwenye chanzo cha maji na sasa wana mkakati wa kupanda miti laki moja katika maeneo hayo na mpaka sasa wamepanda miti zaidi 50,000”Alisema
Hata hvyo alieleza pia wameendelea na mradi wa hati fungani kuongeza uzalishaji maji huku wakieleza mipango yao ni kuongeza uwezo bwawa tuta eneo la kupita utoro wa maji na kazi za mazingira zitafanyika na hivyyo itawasadia kuwa na uhakika wa usambazaji wa maji hata ikitokea mabadiliko ya tabia ya nchi na wakati wa ukame.

Post A Comment: