-Ahimiza Mshikamano katika kujenga Tanzania Imara
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu amesisitiza umuhimu wa kudumisha mahusiano mema ili kuimarisha umoja wa Taifa na kuchochea maendeleo endelevu nchini.
Mhe. Sangu amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Mahusiano kilichofanyika tarehe Februari 24, 2026 katika Halmashauri ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Aidha, amesema kuwa uwepo wa mahusiano imara miongoni mwa Watanzania ni nguzo muhimu ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa.
Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kuratibu na kuimarisha mahusiano baina yake na makundi mbalimbali ya kijamii ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa kielelezo cha utulivu barani Afrika.
Amesema kuwa, sifa ya Mtanzania ambayo ni miongoni mwa sifa kuu zinazomtambulisha ni mahusiano mazuri yanayobebwa na misingi mikuu mitatu, msingi wa kwanza ni mila na desturi za nchi, ambapo, Nchi yetu ina historia ndefu ya ushirikiano na utani kati ya makabila mbalimbali, mifumo ya kisera, kisheria na miongozo mbalimbali ya mahusiano na , umoja na mshikamano ulioachwa na waasisi wa Taifa.
Vilevile, amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila kundi la kijamii kuheshimu na kutekeleza sera na sheria hizo kwa vitendo ili kuendeleza mshikamano wa Taifa.






Post A Comment: