Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ameukaribisha Umoja wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO) na kuutaka kuwa chachu ya kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kupitia utoaji sahihi wa taarifa pamoja na ubunifu wa maudhui.
RC Senyamule ametoa kauli hiyo leo Februari 9, 2026, mara baada ya viongozi wa UMIKIDO kufika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha na kuomba ushirikiano na Serikali ya Mkoa wa Dodoma.

“Hongereni kwa kuanzisha umoja huu. Nimefurahishwa sana kwani utarahisisha kazi na kuwa kiunganishi muhimu kati ya Serikali ya Mkoa na vyombo vya habari vya mitandaoni. Tulitamani kupata watu wanaozungumza lugha moja na Serikali, na tunaamini ninyi ni wazalendo,” amesema Mhe. Senyamule.
Ameeleza kuwa uwepo wa umoja huo utaisaidia Serikali kufikisha taarifa kwa wananchi kwa ufanisi zaidi, sambamba na kuongeza uelewa wa umma kuhusu shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
“Ni muhimu Watanzania wakaendelea kufahamu kazi zinazofanywa na Serikali. Nina imani mtakuwa wabunifu katika kuandaa na kusambaza taarifa kwa njia zitakazowafikia wananchi kwa urahisi,” ameongeza.
Aidha, RC Senyamule amewataka wanachama wa UMIKIDO kuzingatia kutangaza miradi ya kimkakati na mipango ya maendeleo, ikiwemo uhifadhi wa mazingira, matumizi ya nishati safi ya kupikia, sekta ya utalii na michezo, pamoja na kuhamasisha matukio mbalimbali kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Awali, viongozi wa UMIKIDO walieleza dhamira na malengo ya kuanzishwa kwa umoja huo, ikiwa ni pamoja na kuimarisha maadili ya uandishi wa habari za mitandaoni na kushirikiana kwa karibu na Serikali katika utoaji wa taarifa sahihi kwa umma. Pia waliomba ushirikiano kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kutimiza malengo hayo.
Viongozi walioshiriki ziara hiyo ni (Mwenyekiti wa UMIKIDO Bw.Benny Majata,Katibu Emmanuel Charles, Zena Chitwanga (Mhasibu), Daniel Mkate (Afisa Mahusiano), Alex Sonna (Kamati ya Ufuatiliaji), Henry Masanja (Kamati ya Nidhamu) na Ronald Sonyo (Kamati ya Fedha na Mipango).

Post A Comment: