Na Magesa Magesa,Arusha

WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwathamini na kuwajali madaktari na wauguzi hapa nchini kwani wao ndio wamekuwa wakitoa upanyaji kwa wanadamu kwa kupitia kwa Mungu.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT),Dayosisi ya Kaskazini Kati(DKAK)Dk.Godson Abel Mollel ameyasema hayoleo alipokuwa akizungumza na watoa huduma hao wa afya wakati wa kukabidhiwa zawadi kwa kutambua mchango wao.

Zawadi hizo zilitolewa na Mfanyabiashara Nathan Kimaro,alipokuwa akiwapongeza wahudumu hao wa afya wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha,Mount Meru, ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake miaka 27 iliyopita katika hospitali hiyo.

Askofu Mollel amesema kwamba watoa huduma ya afya ni watu muhimu sana katika jamii kwani wao ndio wamekuwa wakiwahudumia wagonjwa wa hali mbalimbali katika mazingira mbalimbali bila kujali changamoto wanazokutana nazo.

“Wakati umefika watanzania tuamke tuhakikishe kuwa tunawajali watoa huduma za afya kwani wao wamekuwa wakitibu na watu kupata kuponywa kupitia kwao kwa uwezo wa Mungu kwani hata Yesu katika wanafunzi wake, Luka alikuwa ni tabibu na yesu alikuwa mponyaji”alisema Askofu huyo.

Kwa upande wake Mfanyabiashara Nathan Mollel aliwashukuru watoa huduma hao wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha kwa kutimiza kikamilifu majukumu yao ya kuwahudumia wagonjwa na kuwataka kuendelea na moyo huo huo.

Alisema kuwa udaktari na uuguzi ni kazi ya wito hivyo hawana budi kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na weledi kama wanavyofanya lakini wahakikishe kuwa wanamtanguliza Mungu kwani yeye ndiye muweza wa kila jambo.

Kahalika mfanyabiashara hyo aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kumpatia eneo lolote lile ambalo atajenga bustani kubwa nay a kisasa itakayokuwa na maua na miti ya aina mbalimbali ambayo itakuwa ikisaidia kuwapa matumani na faraja wagonjwa pindi wanapopumzika katika bustani hiyo.

Katika kusherekea siku yake ya kuzaliwa Nathani Kimaro aliwapatia watumishi wa hospitali hiyovyakula na vifaa mbalimbali ikiwemo,mchele,mafuta,sabuni,sukari,maziwa na kadhalika kama shukrani na kusema kuwa huo ni mwanzo.

Kwa upande wake Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo,Dkt.Abel Ndago alimshukuru mfanyabiashara hyo wa zawadi hizo kwao ikiwemo ahadi yake ya kujenga bustani ya kisasa katika hospitali hiyo

Share To:

Post A Comment: