Kwa muda mrefu nilikuwa nafanya kazi katika kampuni moja ya usambazaji bidhaa, nikiwa msaidizi wa kawaida wa ofisini. Nilimpenda boss wangu kimya kimya tangu siku ya kwanza nilipoanza kazi pale. Alikuwa ni mwanaume mwenye heshima, mwenye busara na aliyevaa harufu ya mafanikio. Nilihisi kuwa ni mtu ambaye kila mwanamke angependa kuwa naye, lakini sikuwahi kufikiria kwamba siku moja ningekuwa sehemu ya maisha yake binafsi.

Kila siku nilijitahidi kufanya kazi yangu kwa bidii, nikihakikisha kila kitu kinachohusu ofisi kiko sawa. Nilimwona akitabasamu kila mara aliponipita, lakini nilijua ule ulikuwa ni tabasamu la heshima, si la mapenzi. Wenzangu kazini walikuwa wanasema ni bure kumpenda boss, maana wanaume kama hao huwa hawataki wanawake wa kawaida kama sisi. Nilinyamaza, lakini ndani ya moyo wangu nilijua kuna kitu tofauti.

Siku moja aliniita ofisini kwake akaniambia, “Naona kazi zako zimekuwa bora sana, endelea hivyo hivyo.” Nilihisi moyo wangu ukicheza kwa furaha. Baada ya hapo alianza kuniamini zaidi, akanipa majukumu mapya. Mara nyingi tulikuwa tukikaa pamoja kupanga mikakati ya kazi, na hapo ndipo nilianza kumjua kwa undani. Alikuwa mpole, mkarimu, lakini pia mwenye mipaka. Nilijaribu kila njia kumvutia, lakini haikuwa rahisi. Soma zaidi hapa 

Share To:

contentproducer

Post A Comment: