Mbunge mteule wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia CCM Chiku Issa Awataka Wananchi wa Arusha Kumpigia Kura za Kishindo Mgombea Urais Dkt. SSH
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Chiku Issa, amewaomba wananchi wa Arusha kumpigia kura za kishindo Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. SSH, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo umefikia asilimia mia moja chini ya uongozi wake.
Akizungumza katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, Chiku Issa alisema:
“Wananchi wa Arusha tumeshuhudia kwa macho yetu jinsi miradi ya maendeleo imeletwa kwenye kila sekta; elimu, afya, maji na miundombinu. Haya yote ni matunda ya uongozi wa Dkt. SSH kupitia CCM.”
Aidha, Mbunge huyo alitumia jukwaa hilo kuwaombea kura wagombea wengine wa CCM mkoani Arusha akiwemo Mgombea Ubunge wa Jiji la Arusha, Paul Makonda, na Mgombea Ubunge wa Longido, Dkt. Stephen Kiruswa, pamoja na madiwani wote wa chama hicho.
“Ili maendeleo haya yaendelee, tunapaswa kumchagua Rais wetu Dkt. SSH, lakini pia tumchague Mheshimiwa Paul Makonda kwa Jiji la Arusha, Dkt. Stephen Kiruswa kwa Jimbo la Longido na madiwani wote wa CCM katika kata zetu. Tukifanya hivyo tutahakikisha Arusha inakuwa ya mfano wa maendeleo nchini,” alisema.
Kwa mujibu wa Chiku Issa, ushindi wa wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani, ni msingi wa kuhakikisha utekelezaji wa Ilani unaendelea kwa kasi na ufanisi zaidi.
Post A Comment: