Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kukamilisha miradi yote ya maji safi na salama pamoja na kuongeza mtandao wa barabara za kiwango cha lami katika Wilaya ya Mbarali na maeneo mengine nchini.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wa Mbarali, Rais Samia alisema serikali itahakikisha barabara ya Kagomba, Ukaguzi na Mtego kuelekea viwandani inajengwa kwa kiwango cha lami, sambamba na kuunganisha mtandao wa barabara katika maeneo ya Igawa, Rujewa, Ubaruku, Chimala, Igurusi, Madibira na Kapunga.
“Tutakamilisha miradi yote tuliyoianzisha na kuhakikisha mipya tutakayoianzisha nayo inamalizika. Tutaimarisha miundombinu ya barabara, reli, usafiri wa anga, usafiri wa majini na madaraja ili kurahisisha biashara na usafirishaji wa watu na mazao,” alisema Rais Samia.
Ameongeza kuwa CCM itaendelea kuimarisha mifumo ya kiserikali na Serikali za Mitaa ili wananchi wa Mbarali na Watanzania kwa ujumla waendelee kufanya kazi kwa bidii na ufanisi zaidi.
Post A Comment: