Mgombea bunge wa Jimbo la Longido,Dkt Steven Kiruswa amewaomba wana Longido kuhakikisha wanamuunga mkono mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} Dkt Samia Suluhu Hassan katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa vyama vingi mwezi Octoba kwa kuwa serikali yake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita imetekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwemo umeme kuwekwa katika vijiji vyote 57 vilivyoko katika kata 20 za Jimbo hilo.

Dkt Kiruswa alisema hayo wakati akichukua fomu ya kuwania ubunge katika ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi{INEC} katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Longido na mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi Mkuu,Nevellng Lyimo na pia alisisitiza katika ofisi ya Chama Wilaya ya Longido kumuunga mkono mgombea Urais wa CCM kwa kuwa wananchi wa Jimbo hilo wana deni kwa mgombea huyo.

Alisema fedha za maendeleo zilizoletwa na Mgombea Urais wa CCM kupitia serikali yake ni fedha nyingi haijawahi kutokea toka Jimbo hilo lianzishwe hivyo shukrani pekee ya wana Longido ni kuhakikisha wanamuunga mkono kwa asilimia mia moja ili tumwonyesha Imani kuwa wananchi wa Longido wanampenda kwa dhati.

‘’Wananchi wa Longido naomba msiniangushe nawaomba tumuunge mkono mgombea wa CCM Wagombea urais wako kumi na saba kutoka katika vyama mbalimbali kwani amefanya mambo makubwa hapa Longido kuhusu miradi ya maendeleo hivyo ni lazima tuwe na fadhila’’alisema

Dkt Kiruswa ambaye aliongozwa na msafara mkubwa wa magari,pikipiki,bajaji na watembea kwa miguu kutoka kata mbalimbali Longido kutoka nyumbani kwake hadi INEC a ofisi za Chama  alisema na kusisistiza kuwa iwapo atachaguliwa tena atamalizia kata tatu kati ya kumi na saba za Jimbo jilo ambazo hajazitekeleza katika miradi ya maendeleo kutokana changamoto mbalimbali ikiwemo elimu.

Alisema pamoja na kumalizia kata hizo lakini bado atahakikisha kila kata ina maji ya uhakika,afya,Barabara nzuri, na mawasiliano ili kila mmoja afurahie maendeleo ya serikali itakayoongozwa na Rais wa CCM kwani ana uhakika atachaguliwa kuiongoza serikali kwa kuwa wananchi wanamwamini na kumpenda.

Naye Mwenyekiti wa CCM Longido,Papa Nakuta alisema  Longido ya sasa sio ile ya zamani kwani Mgombea Urais wa CCM na mgombea ubunge wa Jimbo la Longido wote kwa pamoja wamefanya mambo makubwa kwa ajili ya wananchi wa Longido na kwa hilo amewataka wananchi kulipa fadhila ili wawe wa kwanza Kitaifa kumpa kura Rais ili aweze kuiongoza tena serikali.

Alisema wilaya ya Longido ni wilaya ya kifugaji yenye changamoto nyingi na uhitaji mkubwa wa maji na afya na kufuatia hilo amewaomba wananchi kumpa kura zote Rais na Mbunge wake Kiruswa ili wafanye yale waliyoyapanga katika vipindi vyao vya miaka mitano.

Naye mwananchi wa kata ya Longido,Namnyaki Saiburu alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Longido  watampa kura Rais kwa asilimia mia moja na Mbunge Kiruswa kwani wamefanya mambo makubwa katika Jimbo hilo katika kutatua changamoto kubwa ya maji safi na salama kwa asilimia kubwa.








Share To:

Post A Comment: