Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo vya Habari leo Jumatatu Agosti 11, 2025 katika Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu, Lumumba, jijini Dar es Salaam,kuhusu

harambee ya kuchangia kampeni za chama hicho itakayozinduliwa rasmi kesho katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Harambee hiyo inalenga kukusanya Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya kampeni, ikiwemo gharama za magari, mabango, mafuta, fulana na kanga.
Share To:

Post A Comment: