Na Ferdinand Shayo ,Arusha .


Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kimetoa mafunzo ya utengenezaji wa majiko ya nishati safi pamoja na miundombinu yake kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ili kuwawezesha kutumia nishati hiyo na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni ambayo yanasababisha uharibifu wa mazingira .

Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo ,Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha Felichisim Masawe amempongeza Mkuu wa Jeshi hilo kwa kutoa Maafisa waliopatiwa mafunzo na CAMARTEC ili waweze kutengeneza majiko yanayotumia gesi ya bayogesi pamoja na sufuria.


Masawe amesema kuwa Jeshi hilo limekua mstari wa mbele kutekeleza agenda ya nishati safi kwa kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan ya kuzitaka taasisi zenye watu Zaidi ya 100 kuanza kutumia nishati safi ambapo magereza wameanza tangu mwaka 2024.

Kaimu Mkurugenzi wa CARMATEC Boniface Chatila amelitaka Jeshi la Magereza kuendelea kushirikiana na kituo hicho ili kupata mahitaji yote muhimu ya mitambo ya nishati safi pamoja na kutoa ujuzi kwa Maafisa Magereza ili kueneza Teknolojia hizo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo CAMARTEC Peter Mtoba amesema kituo hicho kimesaini makubaliano ya kutengeneza majiko Zaidi ya 300 ya nishati safi yatakayosambazwa kwenye magereza mbali mbali nchini ili kuhakikisha wanatumia nishati safi na kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa.


Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OKULY BLOG

Post A Comment: