Kwa kweli mapenzi huwa kipimo cha moyo wa binadamu. Nilipokutana na Joel, nilihisi kama ndoto zangu zote kuhusu mwanaume wa ndoto zangu zimefikia ukingoni. Alikuwa mpole, mchangamfu, mkarimu na mwenye ndoto za maisha. Aliniahidi kunioa, alinijumuisha kwa familia yake, na hata alijenga mazingira ya kuonyesha kuwa uhusiano wetu ulikuwa wa kudumu.

Kwa miaka miwili, nilimhudumia kama mke halali. Nilikuwa nikimpikia, kumfulia, hata kusaidia kwenye biashara zake za mtandaoni. Kila alipopata hela, aliniahidi kuninunulia pete ya uchumba na kunipeleka kumtambulisha kwa wazazi wake rasmi. Lakini siku zilikuwa zinapita bila hatua yoyote.

Kilichonitia wasiwasi zaidi ni ndoto za ajabu nilizokuwa nikianza kuota. Mara naota nipo kwenye makaburi nikitawazwa, mara naota nimevaa mavazi ya harusi huku watu wote wamevaa nguo nyeusi za maombolezo. Mwili wangu pia ulianza kuchoka kila mara, usingizi wa mara kwa mara, na kupoteza nguvu ya kuamka asubuhi. Soma zaidi hapa 


Share To:

contentproducer

Post A Comment: