Mgombea Urais kupitia Chama cha ADA TADEA, Georges Bussungu, amesema endapo atachaguliwa kuongoza nchi ataleta mabadiliko makubwa ya fikra, pamoja na mapinduzi ya teknolojia na uchumi kwa Watanzania, akitumia kile alichokiita akili mnemba.

Bussungu amekuwa mgombea wa saba kuchukua fomu za kugombea urais katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), akifanya hivyo leo majira ya saa 8:50 asubuhi. Aliongozana na mgombea mwenza wake, Ali Makame Issa, pamoja na wapambe waliokuwa wakicheza ngoma ya Kigogo kumshangilia.

Hadi sasa, wagombea waliokwishochukua fomu ni pamoja na Samia Suluhu Hassan (CCM), Coaster Kibonde (Chama Makini), Doyo Hassan Doyo (NLD), Kunje Ngombare Mwiru (AAFP), Hassan Almas (NRA) na Twalib Kadege (UPDP).

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, Bussungu alisema serikali itakayoongozwa na chama chake itajenga mtazamo wa usawa kwa jamii na kuendesha kile alichokiita mapinduzi ya njano katika fikra, yakilenga kuendeleza ustawi wa teknolojia na uchumi nchini.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: