Na Magesa Magesa,Arusha

TAASISI ya Global Education Link(GEL)imewataka vijana hapa nchini kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa za kielimu zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha na vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi ili kujiendeleza kielimu pamoja na kupatiwa ufadhili .

Mkurugenzi Mtendaji wa GEL,Abdulmalik Mollel ameyasema hayo leo,alipokuwa akizungumza na wanafunzi na wazazi katika maonyesho ya kimataifa ya vyuo vikuu vya nje ya nchi yanayofanyika mjini hapa.

Mollel amesema kwamba kwa kipindi cha miaka 18 tangu taasisi hiyo ianzishwe imekwisha wapeleka wanafunzi wengi kusoma katika vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi kuwataka watu kuachana na dhana kwamba kusoma nje ya nchi ni gharama jambo ambalo sio kweli.

“Watu wengi wamekuwa na dhana potofu kwamba kusoma nje ni gharama jambo ambalo sio kweli kwani gharama ni sawa na hapa nyumbani hivyo ni wazazi na wanaotaka kusoma nje kuchangamkia fursa hiyo kwani pia kumekuwa kukitolewa ufadhili wa masomo kuanzia asilimia 50 hadi 100,hivyo ni wao kuchangamkia fursa hiyo”alisema Mollel.

Aliongeza kuwa pia taasisi yake imekuwa ikiwapa fursa vijana wa kitanzania kupata ufahamu sio tu anasoma,anasoma kozi gani,chuo na nchi kilichopo kwa gharama nafuu na kwamba wamekuwa wakitoa udahili wa papo kwa hapo ndani ya dakika 15 na ndani ya masaa 24 mwanafunzi anakuwa amekwisha dahiliwa.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa taasisi yake itaendelea kushirikiana na Serikali kuandaa rasilimali watu ili kusidia kuinua uchumi wa nchi na kwamba wao wanataka watanzania wasome kwani elimu ndio msingi wa maendeleo.

Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa ufadhili wa elimu wa  asilimia 100 kwa ngazi ya shahada ya pili,Daniel Kaaya aliipongeza taasisi hiyo kwa kusaidia yeye kupata ufadhili huo wa kwenda kusoma nje ya nchi na kuwataka watanzania wengine kuchangamkia fursa hiyo.

“Niwapongeze sana Global Education Link kwa kuniwezesha kwenda kusoma shahada yangu ya pili katika Chuo Kikuu cha Sharda kilichopo nchini India na niwatake vijana wenzangu wajitokeze sio tu kwenda nje ya nchi bali pia kupata ufahamu wa kazi zitolewazo vyuo na nchi vilivyopo”alisema Kaaya

Katika maonyesho hayo ya Kimataifa ya vyuo vikuu vya nje ya nchi yalioshirikisha vyuo vikuu mbalimbali  wazazi/walezi na wanafunzi mbalimbali walijitokeza kuchangamkia fursa zinazotolewa ambapo wengi waliipongeza Taasisi hiyo kwa kuyaleta maonyesho hayo.







Share To:

Post A Comment: