Jumla ya Washiriki 700 kutoka taasisi mbalimbali za Tanzania bara na Visiwani,wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa Jumuiya ya Wataalamu wa Usimamizi wa Rasilimali watu na utawala katika utumishi wa umma (TAPA-HR ),Unaotarajia kufanyika katika Ukumbi wa kimataifa wa Aicc MkoaninArusha.

Mkutano huo utaanza rasmi Julai  22-25,2025 na kufunguliwa na Waziri wa nchi  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mh George Simbachawene .

Akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo bi.Grace Meshy amesema mkutano huo una lengo la kubadilishana uzoefu katika maswala mbalimbali katika utawala pamoja na kukuza ujuzi na  uweledi na maadili  katika maswala ya rasilimali watu pamoja na utawala.

"Tunafahamu kuwa kada yetu ni kioo cha jamii hivyo tunatarajia kuwa tutaendelea kukumbushana  maadili na kubadilisha uzoefu kwa kuwa jukwaa hili ni la kwanza kufanyika hivyo mambo mazuri yanakuja kwa kuwa sisi ni vioo  katika taasisi zetu"Alisema bi.Meshy

Kauli mbili ya mkutano huo ni mwelekeo mpya wa nafasi ya wataalamu wa usimamizi wa rasilimali watu na utawala kusukuma mabadiliko kuendana na mageuzi ya teknolojia kwaajili ya kuboresha huduma katika utumishi wa umma

Pia  mkutano huo  unalenga kuwakutanisha wataalamu wa kada ya usimamizi wa rasilimali watu na utawala katika utumishi wa umma Kutoka Tanzania bara na visiwani ili  kuwajengea uwezo na  kuleta tija katika kufikisha  malengo makuu ya taasisi zao na ustawi wa wananchi kwa ujumla.

Amewataka  waajiri wote ambao wapo katika wizara mbalimbali Mamlaka za serikali za mtaa, wakala wa serikali pamoja na idara zinazojitegemea kuendelea kuwawezesha wataalamu kuweza kushiriki mkutano huo muhimu .











Share To:

Post A Comment: