Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenan Laban Kihongosi kenani kihongosi amekutana na viongozi wa Dini na viongozi wa mila wa mkoa huo kwa lengo kufahamiana na kupata baraka, dua na maombi kutoka kwa viongozi hao,  ili anapoianza kazi yake iwe na ulinzi wa Mungu, kikao kilichofanyika  kwenye ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa mkoa,  mapema leo Julai 01, 2025.

Amebainisha kuwa, anaamini Mhe.Rais kumleta Arusha si kwa uwezo wake bali ni mpango wa Mungu, na kuwaomba viongozi hao, licha ya kumpa ushirikiano katika utendaji wake kazi, amewasisitiza kuombea amani ya nchi, kumuombea, kumlea, kumfundisha, kumshauri na kumuelekeza pale atakapopotoka ili aweze kuitenda kazi vizuri na kuendeleza mkoa wao wa Arusha.

"Binafsi ninamshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kuja kuwatumikia tena, lakini  katika utumishi wa Umma kuna mambo ambayo yanahitaji msaada wa Mungu, hivyo ninaamini ushauri kutoka kwenu kutokana na umri wangu mdogo, niwaombe viongozi wangu  msiache kuniombea, ninaombe mnilee mimi ni kajana wenu". Ameweka wazi Mhe. Kihongosi.

Aidha, amewaomba kuuombea amani ya mkoa na Taifa kwa ujumla na kuongeza kuwa, waendeleze ushirikiano wao kama walivyoshirikiana na viongozi waliotangulia kwa kuwa mkoa ni ule ule,  kilichobadilika ni uongozi tu lakini malengo ya kuujenga mkoa wetu yako pale pale.

Hata hivyo amewasisitiza kendelea  kuhubiri amani ya nchi yao, kwa kuangalia manufaa ya amani na utulivu, na kuepuka  kujenga chuki na uadui kwa misingi ya dini na vyama vyetu kwa kuweke mbele utaifa hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 

"Viongozi wa dini mnalojukumu la kuiombea Tanzania na viongozi wa mila wanayo kazi ya kuhubiri maadili na amani ya nchi yetu hivyo viongozi wangu ninaomba tushirikiane kuilinda amani, sisi ni watumishi wa Umma, tumekuja kufanya kazi tu, lakini iko siku tutaondoka, hivyo tusikubali kuharibu nyumbani zaidi tuilinde ardhi yetu" Amesema

Tutambue kuwa, Mheshimiwa Rais anayo nia njema kwa nchi yake kwa kuangali mifano ya miradi mikubwa inayotekelezwa nchini katika seka zote hivyo saidieni kuilinda nchi yetu na kumsaidie Mhe Rais.












Share To:

Post A Comment: