NA DENIS MLOWE IRINGA 

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)ITaifa, Injinia Fatma Rembo ametoa wito kwa Jumuiya ya wanawake wilaya ya Iringa Vijijini kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua,kuchaguliwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwani hakuna mwenye hati miliki ya kuongoza.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo Injinia Rembo alisisitiza wanawake hao kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hizo na kuwataka kuhakikisha CCM inashinda kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kumpa kura Nyingi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwani wanawake ndio jeshi kubwa na tegemeo katika kuleta ushindi kwa CCM.

Aidha alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na kushikamana hasa wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao ili kuweza kuleta amani na utulivu nchini.

"Niwaombe sana tunapoelekea kwenye uchaguzi tushikamane tuwe wamoja kwa sababu tunawajibu wa kwenda kutafuta kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan na nina imani wakina Mama wa Mkoa wa Iringa hamtaniangusha tutaibuka kidedea kwa kura za kishindo na Chama cha Mapinduzi kitashinda kwa kishindo" alisema Rembo.

Injinia Rembo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika baraza hilo ambalo lilijadili mikakati ya kuimarisha ushiriki wa wanawake katika siasa na maendeleo na kutoa taarifa wa Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa madiwani katika wilaya hiyo aliwaahidi wanawake wa UWT Mkoa mzima wa kuwashonea sare za uchaguzi ambazo watazitumia katika kampeni za uchaguzi ifikapo Oktoba.


Naye Katibu wa UWT wilayani ya Iringa Vijini. Sophia Nyalusi alisema kuelekea uchaguzi mkuu chama hicho kimepokea maelekezo juu ya zoezi zima la uchaguzi huo na kwamba UWT wilaya hiyo imedhamiria kutoa kura za heshima na za mfano kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema kuwa wanawake mkoani Iringa wanaenda na mama Samia na watampa kura za heshima, mwaka huu 2025 tunataka tutoe kura za mfano kwa mwanamke mwenzetu.

Kwa upande wao wabunge wa viti maalum ,Nancy Nyalusi na Rose Tweve waliwataka wanawake hao kutumia nafssi zao kuchagua viongozi bora ambao watawaletea maendeleo ya uhakika wanawake wa jumuiya na ambao wamekuwa wakiwaunga mkono tangu mwanzo katika changamoto zao.

Wabunge hao walitoa ahadi kwa pamoja pia kuwashonea sare wanawake wa jumuiya hiyo wilaya ya Iringa vijijini ambazo pia watazitumia katika vikao vyao mbalimbali .


Katika baraza hilo la UWT wilaya madiwani wa viti maalum walitumia nafasi hiyo kueleza kwa kipindi cha miaka 5 tangu kuchaguliwa kuwa Utekelezaji wa ilani ya CCM na kushangiliwa kwa kiasi kikubwa kuweza kufanikisha kwa kiasi kikubwa.

Madiwani hao walimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea miradi mbalimbali katika kata zao na kufanya wananchi kufaidika na miradi hiyo ya kimaendeleo kwa kipindi kifupi.
Share To:

Post A Comment: