Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) leo Juni 05, 2024 kimefanya kongamano ili kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Akizungumza katika kongamano hilo, Dkt. Bakari George, Mkuu wa Chuo - TICD, (kwa niaba ya Mhe. Amir Mkalipa, Mkuu wa wilaya Arumeru), ameeleza kuwa dunia inafanya maadhimisho hayo ili kutoa fursa kwa jamii kutafakari umuhimu wa kuhifadhi mazingira duniani.
Dkt. Bakari, ametumia fursa hiyo kuwaeleza washiriki wa kongamano kuwa mara zote, TICD imeadhimisha siku ya mazingira duniani ikiwa ni jitihada ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhimiza na kutilia mkazo ajenda ya utunzaji wa mazingira na ile ya nishati safi inayolenga kuboresha mifumo ya upishi kwa kutumia nishati safi na salama kwa mazingira.
Katika kongamano hilo Athuman Machuma, Faith Kivuyo (ambao ni wanafunzi wa TICD) na Irene Kakiko (Mkufunzi Msaidizi – TICD) wameweza kuwasilisha mada mbalimbali zilizoakisi kauli mbiu kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka 2025 ambayo ni "Kukomesha Taka za Plastiki – kwa Mustakabali wa Sayari yetu."
Prof. George Frank Kinyashi (Naibu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi) na Bi. Janeth Zemba (Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala) waeleza jinsi ambavyo Chuo kimedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu kwa umma juu ya kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Post A Comment: