Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan lei Jumapili Juni 15, 2025 amesisitiza Mahakama ya Tanzania kuendelea kusimamia haki nchini, akiahidi kwamba serikali yake itaendelea kutoa ushirikiano wake kwa muhimili huo.

Dkt. Samia amebainisha hayo wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju, ambaye ameapishwa kuwa Jaji wa saba Mzawa wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye amestaafu utumishi wake.

Katika maelezo yake kwa Jaji Mkuu Mhe. Masaju, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuendelezwa mazuri ya Mahakama hiyo, kuendeleza utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya haki jinai sambamba na kuendelea kusimamia haki ndani ya nchi na haki za Tanzania nje ya nchi.

"Pongezi zangu ni kwa Jaji Mkuu mstaafu kwa kukamilisha kazi hii bila ya makandokando lakini pia jwa Jaji Mkuu mpya nikupongese lakinu pia nikupe pole kwasababu mzigo huu sio mdogo. Una kazi ya kufanya, nakutakia kila la kheri, Mungu akupe busara na hekima uweze kuifanya kazi hii vyema." Amebainisha Rais Samia.

Katika maelezo yake Rais Samia amemshukuru pia Jaji Mkuu Mstaafu Prof. Juma kwa kazi kubwa ya kuleta mageuzi ya kimiundombinu, kimfumo na kiutendaji ndani ya Mahakama suala ambalo ameeleza kuwa limefanikisha kukuza imani ya Watanzania kwa Mahakama yao, akimsihi kuwa tayari muda wowote kutumika tena na serikali pale ambapo itahitajika kutumiwa na serikali.

Amempongeza pia kwa utumishi wake uliotukuka katika kukuza ushirikiano wa Mahakama na mihimili mingine ya Dola sambamba na ujenzi na ukamilishaji wa Makao makuu ya Mahakama ya Tanzania Mjini Dodoma, suala ambalo limewezesha pia Mahakama hiyo kuhamia Dodoma na kuapishwa kwa Jaji Mkuu Mkoani humo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.

Share To:

Post A Comment: