WAZAZI na walezi wametakiwa kutumia fursa ya ujenzi wa miundombinu kwenye sekta ya elimu nchini, kuwahimiza watoto na kuwawezesha watoto Kwenda shule, ili wapate maarifa za stadi za kuwasaidia kwa maisha yao ya baadaye.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ali Ussu, ameyasema hayo leo jijini, baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa madarasa 12 na ofisi kwenye Shule ya Msingi Mbuyuni.
Maradarasa hayo yanajengwa kwa muundo wa ghorofa, ili kutumia eneo dogo lililopo kwa matumizi ya miuondombinu mingi zaidi katika uboreshaji wa elimu.
Ussi amesema Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga miundombinu, uboreshaji huduma na mazingira kwa watumishi wa umma wakiwemo wa sekta ya elimu kama walimu, hivyo ni vema wazazi na walezi wakahakikisha hakuna mtoto anayeshindwa kujiunga, kuendelea na kuhitimu masomo yake.
Taarifa ya Halmashauri ya Jiji la Tanga imeeleza kuwa Shilingi bilioni 5,809,346,807.35 zimetolewa kutoka kwenye mapato ya ndani, ili kutekeleza miradi 84 ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa ya ghorofa, ofisi moja ya walimu na matundu 13 ya vyoo katika Shule ya Msingi Mbuyuni unaogharimu Shilingi milioni 388.8.
“Ujenzi wa madarasa ya ghorofa sio tu utaondoa changamoto ya upungufu madarasa uliosababishwa na ufinyu wa eneo, bali pia utaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia,” imesema taarifa ya mradi huo kwa Kiongozi wa Mwenge 2025,
Imeelezwa kuwa, awali shule hiyo ilikabiriwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, na hii ni kutokana na ufinyu wa eneo ambapo ujenzi wa madarasa ya chini ilikuwa ni changamoto kubwa.
Post A Comment: