Na Mwandishi Wetu, Pangani

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega leo amefika wilayani Pangani mkoani Tanga kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuhani msiba wa mdogo wake Ally Hamidu Aweso aliyefariki ghafla tarehe 9 Mei 2025 mjini Dodoma.

Ulega amempa pole waziri , l Aweso kwa kupatwa na msiba huo wa mdogo wake uliotokea wakati waziri huyo wa maji alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni. 

Ulega ameanza ziara ya kikazi mkoani Tanga na katika tukio hilo la kuhani msiba alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi, Aisha Amour na watendaji wengine kutoka wizarani na Wakala wa Barabara (TANROADS). 

Mdogo huyo wa Aweso amezikwa jana na Ulega alitoa salamu za pole kwa niaba ya wizara na taasisi zake.




Share To:

Post A Comment: