Wafanyabiashara wa Stendi Ndogo Jijini Arusha wameliomba Jiji la Arusha kukaa meza moja na kujadili hoja ya uboreshwaji la eneo hilo badala ya kusikia maneno yasiyo na barua rasmi kutoka kwa watu mbalimbali kuwa kunaujenzi wa ghorofa ya kisasa unatakiwa kujengwa eneo hilo.
Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Angelo Shokia ambaye ni Katibu wa Wafanyabiashara eneo la Stendi Ndogo Jijini Arusha amesema hivi sasa kuna sitofahamu inayoendelea katika eneo hilo pasipo kujua hatma ya wafanyabiashara.
Shokia amesema kuna maneno yanayosambaa kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha kuvunja maduka yaliyojengwa katika eneo la stendi ndogo Arusha lakini hakuna barua yoyote waliyopewa kuhusu uvunjaji wa vibanda vya maduka 400 vinavyonifaisha wafanyabiashara zaidi ya 2000 wakiwemo mamalishe, wachoma mahindi na wengine wanaopanda daladala
"Historia inaonesha kuwa maduka haya yalijengwa na wawekezaji binafsi kufuatia makubaliano ya kimaendeleo kati yao na Jiji,kabla ya ujenzi, eneo hilo lilikuwa makaburi lakini Jiji lilikubaliana na wawekezaji kutoa ardhi, huku wao wakigharamia ujenzi kwa fedha zao. "
Alisema awali halmashauri haikuchangia gharama za ujenzi kwa namna yoyote ile, kila duka lilikuwa lililuwa likilipa kodi ya pango ya sh,200,000 kwa mwezi, ambayo mwezi Julai 2023 kodi ilipandishwa hadi 250,000 kwa mwezi.
Alisema kwa sasa, kuna wawekezaji 400 wanaomiliki maduka hayo kwa kulipa kodi kwa Jiji ya sh,250,000 kila duka huku biashara hizo zikizalisha ajira kwa watu wengi na familia zaidi ya 1,000 zikitegemea mapato yake kwa maisha ya kila siku.
Naye mmoja kati ya diwani wa halmashauri hiyo kutoka Kata ya Ngarenaro Jiji la Arusha, Isaya Doita akizungumzia kuhusu sakata la stendo ndogo alisema hizo ni siasa tu hakuna barua rasmi iliyotolewa na Jiji la Arusha kutoka kwa Mkurugenzi John Kayombo ya kutaka wafanyabiashara hao kuondoka kupisha ujenzi
"Kunakikundi cha watu ambao hawalipi kodi wanaanzisha migogoro isiyo na mag tija ndio sawa eneo hilo lipaswa kujengwa kisasa lakini waonyeshe barua rasmi wanayosema vibanda hivyo vinabomolewa, waache siasa baadhi ya viongozi walipe kodi katika eneo hili na wasitumie siasa kama kichaka kwa kukwepa kodi"
Alisema halmashauri ya Jiji la Arusha linadai kodi zaidi ya sh, bilioni 7 kwa wafanyabiashara hao badala ya kukaa meza moja na wataalam wa Jiji na kilipa madeni wait wanaanzisha migogoro ujenzi utafanyika ila si leo wala kesho ila walipe kodi.
Post A Comment: