Osaka- Japan 26 Mei, 2025
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, ameshuhudia tukio muhimu la utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kampuni ya Axcel Africa.
Tukio hilo lililofanyika katika Kongamano la Uwekezaji kati ya Japan na Tanzania ambalo lilifunguliwa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makubaliano hayo, yaliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa TIC, Ndugu Girald Teri, yanaweka msingi wa ushirikiano madhubuti baina ya TIC na Axcel Africa katika kuvutia wawekezaji kutoka Japan kuja kuwekeza nchini Tanzania. Lengo kuu ni kuongeza fursa za uwekezaji, kukuza uchumi wa taifa na kuleta ajira kwa Watanzania.
Post A Comment: