Muonekano wa Kitengo cha Makasha cha Bandari ya Dar es Salaam kikiwa niaendelea kutoa huduma kwa kutumia vifaa vipya vilivyonunuliwa na Mwekezaji Kampuni ya DP World katika kuboresha huduma kwenye bandari hiyo(.(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Uchukuzi)
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa,akiwasilisha leo Mei 15,2025 bungeni jijini Dodoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
.....
MABORESHO na ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Bandari ya Dar es Salaam umeleta mafanikio ya kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli za kibandari, ambapo katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2024 hadi kufikia mwezi Februari 2025, mapato yatokanayo na Kodi ya Forodha kutoka Bandarini yanayokusanywa kutokana na shughuli za kibandari yamefikia Shilingi trilioni 8.26.
Hayo yameelezwa leo Mei 15,2025 na Waziri wa Uchukuzi,Prof Makame Mbarawa wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumzi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Prof Mbarawa amesema katika kuongeza ufanisi wa bandari, Serikali imeendelea kushirikisha Sekta Binafsi katika uendeshaji wa shughuli za bandari nchini kwa kuingia ubia na Kampuni za DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL)
Amesema lengo la kushirikisha Sekta Binafsi ni kuongeza tija katika utendaji wa bandari nchini ili kuziwezesha zichangie zaidi katika ukuaji wa uchumi wa Taifa letu na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
Amesema wawekezaji hao wamewezesha upatikanaji wa vifaa na mitambo ya kisasa na mifumo ya TEHAMA inayoendelea kuleta ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za kibandari.
Amesema maboresho hayo yameleta mafanikio ya kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli za kibandari, ambapo katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2024 hadi kufikia mwezi Februari 2025, mapato yatokanayo na Kodi ya Forodha kutoka Bandarini yanayokusanywa kutokana na shughuli za kibandari yamefikia Shilingi trilioni 8.26.
“Ni ongezeko la Shilingi trillion 1.18 45 ikilinganishwa na makusanyo ya jumla ya Shilingi trilioni 7.08 yaliyokusanywa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2023/24,”amesema
Pia kumesaidia Kupungua kwa muda wa kusubiri meli nangani kutoka wastani wa siku 46 hadi wastani wa siku saba (7) kwa meli za mizigo mchanganyiko (General cargo) na kichele (Bulk cargo)
“Kupungua kwa muda wa kuhudumia meli za makasha gatini kutoka wastani wa siku 10 hadi siku tatu (3). Kuongezeka kwa wastani wa shehena ya makasha inayohudumiwa kwa mwezi kutoka makasha (TEUs) 17,000 hadi makasha (TEUs) 25,000 ambalo ni ongezeko la asilimia 47,”amesema Waziri Mbarawa.
Pia Kuongezeka kwa makusanyo ya mapato yasiyo ya kikodi yanayokusanywa na taasisi mbalimbali za umma zinazotoa huduma bandarini.
Post A Comment: