Jumla ya washiriki 1,800 wakiwemo Maafisa Elimu Kata 600, Walimu Wakuu 600, na Walimu wa TEHAMA 600 kutoka Halmashauri zote 184 nchini wamejengewa uwezo kuhusu matumizi bora na salama ya TEHAMA katika elimu.

Mafunzo hayo yanatekelezwa na Serikali chini ya Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST), yakilenga kuongeza ufanisi katika kufundisha na kujifunza kwa kutumia TEHAMA.

Akihitimisha mafunzo hayo Aprili, 29, 2025 mkoani Pwani Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Charles Mahera, amesisitiza wanaufaika wote kuhakikisha wanatumia maarifa, vifaa na kuwa wabunifu katika ufundishaji.

Dkt. Mahera amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa matumizi ya TEHAMA katika shule, kuhakikisha vifaa vinatunzwa na kutumika ipasavyo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Awali na Msingi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi Suzan Nussu, amesema shule  800 zitazopokea vifaa vya TEHAMA katika utekekezaji na kuwataka kuvutumia kunuifasha wakimu na wanafunzi kwa ujumla.

Afisa Elimu Kata wa Murusegamba, Ngara mkoani Kagera Bi Catherine Ntente, kwa niaba ya washiriki, amesema mafunzo yamewapa uwezo wa kutumia mbinu mbalimbali za kidijitali kufundisha kiurahisi na kwa ufanisi.










Share To:

Post A Comment: