Na Denis Chambi, Tanga.
TAASISI ya Kuzuia na kupambana na Rushwa 'TAKUKURU' Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuokoa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 76 ambazo ni makusanyo ya mapato ya halmashauri za wilaya za Tanga , Kilindi na Korogwe ambapo watumishi walilopewa dhamana ya kuzikusanya walikosa uadilifu.
Akitoa taarifa ya kipindi cha mwezi Oktoba hadi December 2024 mbele vya vyombo vya habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga Ramadhani Ndwatah amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi walibaini uwepo wa baadhi ya watumishi waliokuwa wakikusanya fedha hizo kinyume na mfumo na hatimaye kuwafikisha Mahakamani ambapo waliamriwa kuzirejesha.
"Miongoni mwa kazi tulizozifanya kwa kipindi hiki tulibaini taarifa za tuhuma za ubadhilifu na ufujaji wa fedha na mali za umma , tuliwafikisha mahakamani watuhumiwa kwa tuhuma za ubadhilifu wakiwa ni watumishi wa umma na Jamhuri ilishinda kesi ambapo waliamriwa na Mahakama kurejesha fedha kiasi cha shilingi Milion 76,048,459.21"
"Katika wilaya ya Kilindi kufuatia Jamhuri kushinda kesi fedha ambazo ni mapato ya Serikali kiasi cha 58,678,780.00 zilirejeshwa, wilayani Korogwe fedha kiasi cha 9,198,045.31 zilirejeshwa ambapo mbali na kurejesha fedha hizo watuhumiwa walipatiwa adhabu nyingine" alisema Ndwatah na kuongeza..
"Katika Jiji la Tanga Jamhuri ilishinda kesi za uhujumu uchumi jumla ya shilingi Bilion 3,171,633.9 zilizofanywa ubadhilifu kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na shilingi 5,000,000 ya mikopo ya asilimia 10 ya wanawake vijana wa watu wenye ulemavu fedha hizo zilirejeshwa na watuhumiwa kwa amri ya Mahakama sambamba na adhabu nyingine."
Aidha Ndwatah ameeleza kuwa TAKUKURU katika kutekeleza jukumu lake la kiuchunguzi imepokea jumla ya taarifa 120 ambapo kati ya hizo 82 zilihusu vitendo vya rushwa na 38 hazikuhusiana na vitendo vya rushwa huku 76 zikiendelea kuchunguza wakati huo huo 38 zimefungwa na nyingine 6 zikihamishiwa idara nyingine.
Ndwatah ameongeza kuwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga imejipanga katika kipindi cha January hadi Marchi 2025 kuendelea kufwatilia miradi ya maendeleo ikiwemo ya Barabara ,huku ikichukua hatua kali za kisheria ili kudhibiti mianya ya rushwa.
" Mikakati yetu ni kuendelea kufwatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya Barabara na mingineyo , tutaendelea kufanya udhibiti na uzuiaji kwenye eneo la ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana na mamlaka husika.
Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga amewataka wananchi na jamii kwa ujumla kuendelea kuwa wazalendo kwa kutoa ushirikiano pale wanapoona viashiria vya rushwa kutoa taarifa kwenye Mamlaka husika.
"Ninatoka wito kwa wadau wote kuendelea kutekeleza kauli mbiu yetu isemayo kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anazuia vitendo vya rushwa katika eneo lake" alisema.
Katika hatua nyingine taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa "TAKUKURU " Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuwafikia wananchi 1,489,269 kupitia mikutano ya hadhara , maeonyesho mbalimbali , mashuleni , watoa huduma wakiwemo watumishi wa Serikali ikiwa ni mkakati wake kwa jamii kueleza kuhusu athari za kutoa na kupokea rushwa .
Post A Comment: