Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga ambae pia ni Mjumbe wa kamati kuu Taifa Rajab Abrahamani amefanya mkutano na kuzungumza na wananchi na kuzindua matawi ya CCM katika eneo la soko la Mgandini na kuahidi kutatua baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika kuendeleza biashara zao.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Rajab amesema serikali ina mipango mikubwa kwa maendeleo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu rafiki kwao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuimarisha utendaji kazi wa mwananchi mmoja mmoja katika kujiimarisha kiuchumi. 


Nae Mkuu wa mkoa wa tanga Balozi Dkt Batilda Buriani pamoja na Mstahiki meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow walipata nafasi ya kushiriki katika suala zima la kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na mwenyekiti Rajab na kuahidi  kutatua changamoto za wafanyabiashara hao.

Share To:

Post A Comment: