Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma kwaajili ya kufungua Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini tarehe 09 Septemba 2024.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki katika Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2024. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya jitihada za uhifadhi wa mazingira kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) wakati wa Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2024.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapongeza Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mnadan ya mkoani Dodoma mara baada ya kuimba wimbo wa kuhamasisha utunzaji mazingira katika Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati akifungua Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na baadhi ya madereva wa bajaji na pikipiki kuhusu usalama barabarani na uhifadhi wa mazingira mara baada ya kufungua Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, amewataka viongozi, wataalamu, na wadau wa mazingira kushirikiana kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto za kimazingira nchini. Dkt. Mpango alitoa wito huo alipokuwa akifungua Mkutano Maalum wa Mazingira uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, mkoani Dodoma.

Katika hotuba yake, Makamu wa Rais alisisitiza kuwa, licha ya mafanikio yaliyopatikana katika kuweka sera na kanuni za mazingira, utekelezaji wa sheria na maelekezo umekuwa hafifu katika ngazi za chini kama vile Mikoa, Halmashauri, na vijiji. Hali hii inatokana na mapungufu ya kisheria, hususan nguvu na wigo wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Dkt. Mpango alielezea umuhimu wa elimu kwa umma kuhusu biashara ya hewa ya kaboni, akibainisha kuwa Tanzania ina masinki makubwa ya kaboni, kama vile ardhi oevu, misitu, na maeneo ya hifadhi. Aliongeza kuwa, nchi zinazoendelea kama Tanzania zinahitaji kufahamu haki na wajibu wao kwenye mikataba ya kimataifa kuhusu hewa ya kaboni na kujiandaa kutumia fursa hii kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Makamu wa Rais alisisitiza umuhimu wa utafiti zaidi katika dhana ya uchumi wa buluu ili kubaini fursa zilizopo katika rasilimali za maji, ikiwa ni pamoja na gesi asili, madini, na viumbe wa baharini. Pia alielezea changamoto mbalimbali za mazingira zinazosababishwa na shughuli za kibinadamu kama ukataji miti hovyo, uharibifu wa vyanzo vya maji, na uchafuzi wa mazingira.

Serikali, alisema, inafanya juhudi mbalimbali za kukabiliana na uharibifu wa mazingira kupitia sera, mikakati ya upandaji miti, na kampeni za usafi. Hata hivyo, alibainisha kuwa juhudi hizo zinakumbana na changamoto kama sheria kinzani, uhaba wa vitalu vya miti, na ukosefu wa miundombinu ya kutosha ya ukusanyaji wa taka.

Mkutano huo wa siku mbili unalenga kujadili hali ya mazingira nchini na kuhamasisha taasisi za umma, sekta binafsi, na asasi za kiraia kuhusu wajibu wao katika kulinda na kutumia rasilimali za mazingira kwa njia endelevu.

Share To:

Post A Comment: