Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Lemomo Kiruswa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Marko Ng'umbi.

Dkt. Kiruswa amesema kuwa Wilaya ya Longido imepata heshima kubwa kutoka kwa Rais Dkt. Samia kumtengua aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye alidhalilisha uongozi wa Wilaya kuanzia viongozi wa mila,Chama pamoja na Watumishi wa Halmashauri kwani aliwaburuza vibaya na walimvumilia nakumlea kwani jamii ya kimaasai inausikivu mkubwa na inapenda sana amani,nidhamu na hekima.

"Ila kwa kauli zake mwenyewe kaja kukitukana Chama cha Mapinduzi na Serikali kwamba ilibeba uchaguzi wa mkuu 2020 jambo ambalo sio la kweli kabisa,Wilaya hii ni ngome ya CCM na imetamalaki tangu mzee Lekule alipoanzisha wilaya hii watu wote wanashinda kwa haki na kwa kufuata utaratibu katika wilaya hii"Ameongezea Kiruswa

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Wilaya ya Longido Salum Kali akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kilimahewa Kata ya Mundarara amesema amejipanga kuwatumikia wananchi na kwamba namba yake ya simu anayogawa kwa wananchi itapatikana saa 24,na kwamba muda wote wamwambie kero na atawafikia.

"Naomba niwahakikishie wilaya yenu ipo salama.Kero zenu nimezisikia suala la daraja Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) watakuja,pia mmesema kuna shida ya zahanati na kituo,"amesema.

Nitapita kijiji kwa kijiji,serikali inapaswa iwepo itatue kero zenu,mmesema mnashida ya malisho mimi ni mwakilishi wa Rais Samia Suluhu Hassan, nitahakikisha nasimamia vizuri na kutatua kila kero,ni wajibu wetu kama viongozi wa serikali.


Akizungumza katika Mkutano wa hadhara katika Kata ya Mundarara Katibu wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM,Amos Makalla,amewaomba radhi wanachi wa Longido kwa kauli ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marco Ng'umbi kwamba zililenga kuwachonganisha kwani Chama cha Mapinduzi kinaheshimu uchaguzi wa haki na kushinda kwenye sanduku la kura na sio vinginevyo

"Yale maneno yameshapita,zile zilikuwa kauli zake yeye,sijui alienda porini kufanya nini kama alienda kutafuta shamba au kuchimba dawa anajua yeye,"amesema.

Amesema CCM inajivunia utekelezaji wa Ilani ya CCM,hatuhitaji mbeleko,hapa ni ngome yetu hivyo hakukua na sababu za kutofuata misingi ya uchaguzi.












Share To:

Post A Comment: