Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla amesema hayo wakati akizungumza Katika kikao cha ndani na Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa Arusha
“Nimekuja Arusha kwa ajili ya kumalizia maeneo ambavyo wakati tunakuja kwenye ziara ya Katibu Mkuu hatukufika Ngorongoro,Karatu na Monduli ,lakini niliomba nafasi kwenda Ngorongoro kuzungumza na wananchi lakini tulivyoomba kibali tulikatazwa na sababu sie ni Chama kiongozi tumekubali na wenzetu wajifunze kwetu na hii ni Ujumbe kuwa tunaheshimu utawala wa kisheria”.
“Hata yule jamaa wa Longido aliyoyasema sio maneno ya Chama mie kama Msemaji wa Chama niseme yalikuwa maneno yake na ukimsikiliza alikosa hoja huko vichani sijui alifata nini sisi Chama cha Mapinduzi hatujamtuma na hatuhusiki na maneno sisi tunajipanga kushinda kwa haki na imekuwa kawaida ya kushinda kwa haki hivyo niwaambie Wananchi na Watanzania yalikuwa maneno yake na sio msimamo wa Chama”.
"CCM inashinda Chaguzi zake kwa haki na sio Kwa kubebwa bebwa na itaendelea kushinda kwa sababu tumejipanga vizuri kushinda chaguzi zijazo" Alisena
"Sisi ni Chama kiongozi tumekubali kutokwenda Ngorongoro wenzetu waige Mfano wetu" Makalla
Post A Comment: