Kituo kikubwa cha umeme chajengwa wilayani Kongwa

Kuimarisha umeme hadi Gairo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mfumo wa gridi ya Taifa una umeme wa kutosheleza mahitaji ya kijamii na kiuchumi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Agosti 02, 2024 wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi. 

Ameeleza kuwa, Serikali inazidi kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ambapo imejenga kituo cha kupokea na kupoza umeme wilayani Kongwa mkoani Dodoma ambacho  kitaboresha pia  hali ya umeme wilayani Gairo.

Ameongeza kuwa, njia ya kusafirisha umeme kutoka kituo cha kupoza umeme cha  Kongwa kwenda wilayani Gairo imeshakamilika.

Share To:

Post A Comment: