1000267651

Watumishi wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), wamenolewa kwa kupata mafunzo yanayohusu utoaji na upokeaji wa rushwa kutoka kwa wadau mbalimbali.

Mwenzeshaji, Bi. Felista Banda, ambaye pia ni Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi wa TANROADS, amesema mada hii ni muhimu kufundishwa mara kwa mara kwa kuwa inawakumbusha watumishi katazo la upokeaji au utoaji rushwa, kwani kufanya hivyo kunadhoofisha utendaji kazi wa mtumishi husika na taasisi kwa ujumla.

Bi. Banda serikali kupitia taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Oktoba mwaka 2023 umezindua mkakati na mpango wa utekelezaji wa awamu ya nne utakaofanya kazi hadi mwaka 2030, ukiwa na lengo la kukuza uadilifu na kupambana na rushwa nchini.

1000267655

Amesema kwa upande wa TANROADS umeunda kamati ya uadilifu itakayoshughulikia masuala yote yanayohusiana na uadilifu katika taasisi ikiwemo ya watumishi watakaobainika kufanya vitendo vya upokeaji na hata utoaji rushwa kwa ajili ya kupata huduma fulani, kwa kutofuata taratibu kwa manufaa yao binafsi.

Bi. Banda amesema kamati hii ya uadilifu imeandaa mpangokazi wa kutekeleza kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kubainisha maeneo yenye viashiria vya rushwa na kuandaa afua za kushughulikia changamoto hizo ndani ya taasisi.

“Kamati ya uadilifu baada ya kumaliza kazi endapo itapata watumishi wenye kuvunja miiko na uadilifu kwa serikali wanawajibu wa kuwasilisha kwenye menejimenti ya taasisi kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi na kutolewa maamuzi,” amesema Bi. Banda  

Mbali na masuala ya rushwa pia watumishi wamefundishwa madili ya utendaji kupitia kanuni nane za maadili katika utendaji kazi wa utumishi wa umma, wanazopaswa kuzifuata zikiwemo za kutoa huduma bora, utii kwa serikali na kutuma huduma bila upendeleo.
 
  “Hizi kanuni zinatukumbusha watumishi wa umma kama vile serikali inavyotutaka kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa jamii, hivyo hatuna budi kuziishi bila kuzivunja au kuzikiuka ili serikali iweze kutoa huduma bora kupitia taasisi yetu ya TANROADS kwa jamii,” amesema Bi. Banda
1000267653
1000267649
Share To:

Post A Comment: