Antonia Raphael mwakilishi wa Mkurugenzi Wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii
Washiriki wakiwa makini kumsikiliza Antonia Raphael mwakilishi wa Mkurugenzi Wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii

Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Halmashauri  za Wilaya  91 nchini zinazokabiliwa na migongano kati ya binadamu  na wanyamapori  wakali na waharibifu, ambapo imekuwa ikipata madhara mbalimbali ikiwemo uharibifu  wa mashamba hekari mia mbili themanini  katika vijiji kumi na nne na  watu wawili kupoteza maisha katika kipindi cha mwaka 2023-2024.


Hayo yamebainika  na mwakilishi  wa Mkuu wa Wilaya ya  Manyoni, Leila Sawe ambaye pia ni Afisa Tawala wa Wilaya hiyo,  wakati wa ufunguzi  wa mafunzo  ya utatuzi wa migongano kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu yaliyoendeshwa na Wizara ya Maliasili na Utalii ikihusisha taasisi zake za TAWIRI, TAWA, TFS na wadau  wa UNDP.


Sawe amewataka Viongozi wa Vijiji na wananchi kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ya siku tatu kwa nadharia na vitendo na kuwa mabalozi wazuri kutoa elimu hiyo kwa wanachi wengine


" niwasihi tuache utamaduni  wa mazoea ya kuhudhuria mafunzo bila kuyafanyia kazi" amehimiza Sawe


Naye, mwakilishi wa Mkurugenzi wa wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na utalii  Antonia Raphael amesema kuwa,  migongano baina ya binadamu na wanyamapori ni changamoto katika  uhifadhi  na katika kuitatua Wizara  ya  Maliasili  na  Utalii  inatekeleza mkakati wa kuzuia changamoto hiyo ambapo utoaji mafunzo kwa wananchi ni kipengela kimojawapo  kati ya vipengele saba vya mkakati huo.


Naye, Mwenyekiti  wa  CCM  Wilaya  ya  Manyoni Bw.Jummanne Makanda ametoa wito kwa wananchi kutumia mafunzo hayo ili kuimarisha  uhifadhi  na  kukuza  utalii  nchini

 " babu zetu walihifadhi rasilimali  hii ya wanyamapori  ndio maana leo  tunanufaika na mapato ya Utalii  na kujivunia fahari ya kuwa na wanyama hawa, hivyo nasi hatuna budi  kuwahifadhi " amehimiza Makanda.


Kwa niaba ya Wananchi wa Manyoni,  Diwani wa Kata ya Mjini Mhe. Saimon Mapunda ameishukuru  Serikali  kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuwezesha mafunzo ya utatuzi wa migongano  kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waaribifu  ikiwa ni mwitikio wa kilio cha wananchi  cha madhara  yanayosababishwa  na wanayamapori  hususani  Tembo 


Aidha, Mafunzo ya utatuzi wa migongano  kati ya  binadamu  na  wanyamapori  wakali  na  waharibifu  ambayo yanatolewa na Wizara  ya  Maliasili  na  Utalii  na taasisi  zake  za  TAWIRI, TAWA, TFS  pamoja na wadau wa UNDP yanaendelea kwa siku tatu ambapo baada ya wananchi kupata mafunzo  kwa nadharia  wapo uwandani kwa mafunzo ya Vitendo

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: