Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Benedict Ndomba akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili wa juu matumizi ya mifumo,jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa UABA Yaliwe Mlambo akizungumza umuhimu wa mifumo ya mawasiliano kwa Taasisi , jijini Dar es Salaam.


Mtaalamu wa Mifumo Matt Nowakowski akizungumza kuhusiana namna Teknolojia inavyokwenda kwa Kasi ,jijini Dar es Salaam.



Ndomba amesema wanaendana na dunia katika katika kufanya utafiti wa teknolojia ya mifumo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imekutana na wadau katika mwenendo wa matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya mawasiliano katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Benedict Ndomba amesema kuwa katika teknolojia mpya ya 'Blockchain' inafanya kuwa taarifa kutokuwa sehemu moja ambayo inasaidia kila mtu kwenye mzunguko kupata taarifa hiyo.

Amesema kuwa Taasisi za Umma wakitumia mfumo wa Blockchain kutafanya huduma kuwa bora kutokana na taarifa kutokuwa mtu mmoja.

Aidha mfumo mwingine sarafu za kidijiti ambao utarahisisha namna kutoa huduma za kifedha na miamala kwenye Taasisi za Umma Kwa kushirikiana na Taasisi fedha zikiwemo Benki.

Amesema kuwa Teknolojia za Mawasiliano na mifumo ya Teknolojia inabadilika ambapo Mamlaka lazima kwenda nayo kwa ajili ya kuhudumia Taasisi za Umma katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Kama Mamlaka lazima tuone mbali kuhusiana na mifumo ya mawasiliano katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Mawasiliano na Taasisi za Umma bila kikwazo na huduma hizo wanapata kwa wakati"amesema Ndomba

Amesema kuwa wamekutana kupata uelewa kwa pamoja na taasisi za Umma na mashirika ambayo yako na mifumo hiyo.

Ndomba amesema katika teknolojia kutokuwa sehemu moja kutaondoa udanganyifu baadhi watoa huduma.

Amesema e-GA wanendelea kufanya utafiti kwenda na dunia na usalama teknolojia ya mawasiliano. Mwenyekiti wa UABA Yaliwe Mlambo amesema kuwa wameamua kushirikiana na Tanzania kutokana na kuwa mbele katika teknolojia ya mifumo.

Share To:

Post A Comment: