Waziri wa Elimu ,Sayansi na Tkenolojia,Mhe. Prof.Adolf Mkenda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya shindano la pili la stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa shule za Msingi nchini ambalo litafanyika kesho tarehe 25/06/2024 jijini Dar es salaam.


Shindano hilo linaandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) kwa ufadhili wa benki ya duniani ambapo jumla ya walimu 21 kutoka nchi nzima walifanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la stadi za ufundishaji wa somo la Kiingereza.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET)Dkt Aneth Komba amesema kuwa lengo la shindano hilo ni kuendelea kuwapa motisha walimu katika kazi zao na kwamba mwaka huu uitikio umekuwa mkubwa kwa walimu kushiriki katika kutuma kazi zao wakiwa wanafundisha.

“Kwa kweli shindano hili linaleta hamasa kwa walimu nchini, tunashukuru walimu wote waliojitokeza katika kuleta kazi zao zikafanyiwa tathimini”amesema , Dkt.Komba.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni tatu,mshindi wa pili shilingi milioni mbili na nusu, mshindi wa tatu shilingi milioni mbili na mshindi wa nne hadi wa kumi atazawadiwa kiasi cha shilingi laki tano.
Share To:

Post A Comment: