Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndugu Mohamed Kawaida ameitaka Serikali kuufungia mtandao wa ‘X’ (twitter) kwa kile alichodai kuwa mtandao huo umeruhusu machapisho ya ngono na mambo yaliyokinyume na mila na desturi za Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa Habari Kawaida amekemea na kulaani vikali vitendo vya ushoga huku wakitaja baadhi ya mitandao ya kijamii imekuwa chanzo cha kuchochea jambo hilo.

Kawaida ameiomba serikali kuweza kufungia mtandao huo mbao upo na maudhui ambayo yanakinzana na utamaduni wa taifa letu.

Hata hivyo Ndugu Kawaida amesema jambo hilo halikubakiki hata kidogo na kwamba umoja huo watapinga kwa nguvu zote juu ya vitendo hivyo viovu.
Share To:

Post A Comment: