Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) amewasihi Maafisa Usafirishaji (Madereva Bajaji na Bodaboda) wa Manispaa ya Tabora waliojitokeza kumpokea alipokuwa akiwasili mkoani hapo kuhamasisha ushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji na kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura.
"Kwa Heshima kubwa nitoe salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, licha ya kuwa ni Rais pia ni Mama na amehakikisha anatubeba vijana kwenye mbeleko yake kwa kutoa fursa kwa vijana kwa kututoa mtaani na kutupeleka site kwa mikopo ya Halmashauri 10% na programu za BBT mfano ni bajeti ya kilimo iliyobeba ajenda kubwa ya vijanab, kwa hakika mama ni mpambanaji".
"Dkt Samia anatukumbusha kuwa waadilifu, kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki katika agenda kuu ya uchaguzi Kwa mwaka 2024/2025".
"Hivyo ndugu wana Tabora niwasihi sana kuendelea kuupeleka ujumbe kwa abiria mnaowabeba kuwa CCM pekee ndiyo inauwezo wa kuzibeba changamoto za maafisa usafirishaji na Watanzania na kuzipatia utatuzi".
Aidha Komredi Rehema Sombi alifikisha salamu za Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu. Mohammed Ali Kawaida (MCC) na Katibu mkuu UVCCM Ndg. Jokate Urban Mwegelo(MNEC).
Post A Comment: