NA HADIJA OMARY, RUVUMA 


Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na utalii imeendelea kujenga vituo  kupeleke asikali wa wanyama poli pamoja na vitendea kazi Katika maeneo yote yenyechangamoto ya wanyama wakali na walibifu aina ya Tembo ili kukabiliana na changamoto hivyo


Hayo yameelezwa na Mratibu wa Mradi wa kutatua changamoto ya migongano baina ya binaadamu na Wanyama poli unaotekelezwa Katika wiliya za Liwale Mkoani Lindi, Namtumbo na Tunduru Mkoani Ruvuma Bw.Gideon Mseja alipokuwa anafungua mafunzo ya siku moja kwa waadishi wa vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika huko Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma


Mafunzo hayo yamewakutananisha waandishi 10 kutoka Katika Maeneo ya utekelezaji wa Mradi maafisa habari wa halmashauri , wawakilishi kutoka kitengo cha  mawasiliano wizara ya maliasili na utalii pamoja na maafisa Wa Serikali Amesema changamoto hiyo ya wanyama wakali na waaribifu imeathi Katika wilaya 44 ambapo Serikali imeendelea kuchukua Hata mbalimbali Katika kukabiliana nayo ikiwa pamoja na kufanya Doria za mara kwa mara kujenga vituo vya asikali wanyama poli.


Jitihada zingine ni pamoja na kuwezesha vifaa vya kuondoa tembo maeneo ya wananchi, kufuatilia miendendo ya wanyamapori, kutumia helikopta na mabomu baridi kuwaondoa tembo kwenye makazi, kuwezesha wananchi kiuchumi na kutoa elimu ya tabia ya tembo na mbinu ya kutatua migongano hiyo kwa jamii ili kujenga uhimilivu wa matukio hayo.


"Lakini pia Serikali imekuwa ikifuatilia mienendo ya wanyama kuona mzunguko wao ambapo  kupitia  TAWILI Tembo wamefungwa vifaa ili vinavyoweza kutoa taarifa mapema endapo wanyama wanakaribia Maeneo ya Jamii basi asikali waweze kusogea pale ili wanyama hao wasisababishe madhara kwa wananchi"


Hata hivyo ameongeza kuwa Katika kuendelea kukabiliana na changamoto hivyo Serikali imeanzisha Mradi wa mashirikiano kati ya Tanzania na ujerumani unaolenga kutatua migongano baina ya Binaadamu na Wanyama poli  unaotekelezwa kwenye ukanda wa Ruvuma unaolenga kutoa elimu ya namna sahihi ya kuandika habari zinazohusu migongano hiyo  kwa usahihi


Kwa upande wake Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari za mazinginra (JET) Bw.John Chikomo amesema Mradi huo wa kudhibiti migongano baina ya binadamu na Wanyama poli upo chini ya   wizara ya maliasili na utalii kupitia ufadhiri  wa Serikali ya Ujerumani  (MBZ) kupitia Shirika la maendeo la ujerumani (GIZ) unatekelezwa na (JET) kwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuripoti vyema habari za hizo za migongano baina ya Binaadamu na Wanyama pori


"Mradi huu utawawezesha waandishi wa habari kuweza kuandika habari hizo kwa usahihi ili wananchi wanaoishi Katika Maeneo ya shoroba za wilaya hizo tatu wapate uelewa wa kujua namna gani ya kupambana na hiyo Hali ambayo wanakutana nayo"


" Ni wazi kuwa maswala haya ya migongano baina ya binadamu na Wanyama pori yamekuwa ni mengi kwenye magazeti tunasoma, kwenye TV tunaona kwamba Kumekuwa na ongezeko la wanyama kuingia Katika Maeneo ya makazi , mashamba kwa hivyo lengo kubwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Tanzania hususani wa wilaya hizi waweze kuandika habari za ufasaha zaidi bila kuleta tahaluki kwa wananchi hao" alisema Chikomo
Kwa Upande wake Mtaalam Mshauri wa Mradi huo  wa kutatua  Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori kutoka  Shirika la maendeo la ujerumani GIZ, Bi. Ana Kimambo alitumia fursa hiyo kuwahasa waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo , kuyatumia mafunzo hayo Katika kuleta matokeo chanya Katika Jamii zao kwa kuandika habari zenye usahihi
" Baada ya mafunzo haya tutapenda kuona sasa taarifa zile zinazo ripotiwa hasa  ukanda huu zinakuwa na mabadiliko ya kuelimisha zaidi pamoja na kufikisha ujumbe wa uhalisia , hakiiisha unachokiandika  unaandika kwa usahihi kulingana na taarifa yenyewe ilivyo"


Kumekuwa na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya waandishi wa habari ambao ndio unaozua tahaluki kwa wananchi na hiyo ndio inayopelekea wananchi wawezekuona kuwa haya matukio kwamba yanaukubwa zaidi tofauti na uhalisia wenyewe  usiiandike Tu kwa sababu unataka gazeti lako liweze kuuza,  amesema waandishi hao wanapatiwa mafunzo hayo ili wanapoenda kwenye Jamii waweze kuielimisha kwa ufasahaKwa upande wake Joyce Joliga mwandishi wa habari wa Gazeti la mwanachi amesema kupitia mafunzo hayo ameeleza kujifunza namna Bora ya kuandika habari hizo za migongano ya Binaadamu na Wanyama poli kwa weledi tofauti na hapo awali ambapo alikuwa akiandika habari hizo kwa kutumia uzoefu wa uandishi wa habari kimazoea
Mwisho

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: