MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Chacha Wambura anayetoka Mkoa wa Geita , ameitaka jamii kujenga tabia kutunza mazingira kila siku kwa kufanya usafi huku akiwapongeza taasisi ya Wanawake na Samia kwa kuwa mabalozi wema wa utunzaji wa mazingira na kuhamasisha usafi kwenye jamii.
Mnec Chacha ametoa wito huo wakati akiwa ni mgeni rasmi Mapema Leo tar 6 June 2024 kwenye shughuli ya kusafisha wa mazingira Mjini Geita ,Shughuli ambayo imeratibiwa na taasisi ya wanawake na Samia.
Amesema suala la utunzaji wa mazingira na usafi ni suala ambalo lazima mtu yoyote ajengewe tabia ya kupenda kujua umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa vizazi vijavyo na vya baadae.
“Niwapongeze sana taasisi ya wanawake na Samia kwani nimewaona mara kadhaa mmekuwa mstari wa mbele kuhamasisha sera ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira najua shughuli hii mnaifanya kwa kupenda na kutoka moyoni niwahaidi mimi nitakuwa na nyinyi muda wowote kuwasaidia kutimiza ndoto yenu kubwa mliyonayo ya kuona watu wanakuwa na mwamko wa kutunza mazingira”Chacha Wambura MNEC Taifa.
Aidha Mnec Chacha amehaidi kukaa na Halmashauri ya Mji wa Geita kwa lengo la kuongeza ulinzi kwenye viwanja vya maonesho ya epz hili kudhibiti vitendo vya wizi wa miche ambavyo vimekuwa vikifanywa na kupelekea kurudisha nyuma jitihada za uwifadhi na utunzaji wa miti ambayo imependwa na taasisi hiyo.
“Mimi nitasaidia walau gharama za kurekebisha maeneo haya ya EPZ ambayo mmependa miti kwa kudhibiti uchomaji wa moto ambao unapelekea kuungua kwa miti pamoja na kuweka ulinzi ambao utasaidia miti ambayo mmeipanda kukua na kuwa imara” Chacha Wambura MNEC Taifa.
Naye Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Halmashauri ya Mji wa Geita,Lee Joshua akitoa taarifa ya utekelezaji wa agiza la upandaji wa miti amesema halmashauri ya Mji wa Geita imefanikiwakupanda miti zaidi ya Milioni Moja.
“Pamoja na kupanda miti tumeendelea kuwasisitiza wenyeji wa maeneo haya kuwa mstari wa mbele katika kutunza miti ya asili jitihada hizi lengo lake ni kuhakikisha tunatunza uoto wa asili kwenye mji wetu wa Geita na kuufanya kuwa mji wa Kijani” Lee Joshua Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Halmashauri ya Mji wa Geita.
Mwenyekiti wa taasisi ya wanawake na Samia Adelina Kabakama amebainisha changamoto ambazo wameendelea kukumbana nazo katika shughuli ya utunzaji wa mazingira likiwemo suala la upandaji wamiti ni baadhi ya watu kutokuwa wema ambao wamekuwa na tabia ya kuiba miti na wengine kuichoma suala ambalo linawarudisha nyuma kiutendaji pamoja na baadhi ya watu wamekuwa wakipitisha mifugo kwenye eneo ambalo limepandwa miti.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Chacha Wambura akishiriki zoezi la umwagiliaji wa mti mara baada ya kuupanda.
Post A Comment: