Unajua kwamba kuna wafanyabiashara 5 tu nchi hii wanaweza kuchezesha bei ya sukari iwe wanavyotaka ili wapata faida ya kufuru? Yes. Watano tu unawahesabu kwa mkono wako mmoja. Watu 5 wanaamua bei ya bidhaa muhimu kwa mamilioni ya Watanzania masikini.
Vinara wawili kati ya hao watano wenye roho ngumu zaidi ni Mohammed Enterprises & Super Doll! Tena wanalindwa na sheria kwamba wana uwekezaji kwenye viwanda hivyo basi lazima wapate haki ya kuagiza sukari ili kulinda viwanda vyao.
Serikali ilipoona sukari inakwenda kuwa shilingi 6,000 ikaamua kutoa vibali vya kuagiza kwa kampuni zaidi kwa dharura ili kuinusu nchi.
Maana waagizaji wakiwa wa kutosha, sukari inashuka bei. Wao wanataka waagize wao tu ili wapange kiasi cha sukari kilichopo kwenye mzunguko na bei.
Basi baada ya hatua ya serikali kuivunja hiyo nguvu yao kwenye maisha ya mamilioni ya Watanzania mabepari hao wakaona ugali wao umevamiwa, kitumbua kimeingia mchana!
Wanafanyaje?
Sasa wanawalipa watu kama kina Luhaga Mpina kupiga mishale hatua zile ambazo serikali ilichukua kuinusu nchi na makucha yao ya uhujumu wa maisha ya Watanzania kupitia bei ya sukari.
Hivi CCM mnamuona Mbunge wenu anavyolipwa kuponda moja ya uamuzi muhimu kuwahi kufanywa na serikali kunusuru Watanzania? Huyu hamuwezi kumuita akahojiwa na kuchuliwa hatua? Mbona taarifa za namna kundi la watu hao watano wanavyowanyonga Watanzania kwenye bei ya sukari miaka nenda rudi ziko wazi? Wako wapi Wabunge na viongozi wa CCM kulisema hili na kusimama na Watanzania? Mnataka Watanzania tubakie mateka wa bei ya sukari kwa watu hao watano mpaka lini?
Mwalimu Robi Kengete
Safarini Mpindimbi Masasi
Post A Comment: