Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewasihi Vijana wasomi wanaohitimu Elimu ya Vyuo na Vyuo Vikuu kuchangamkia fursa ya mikopo ya Halmashauri ambayo Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameifanyia maboresho makubwa.

Komredi Kawaida ameyasema hayo alipokua anahutubia wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam kwenye Mahafali ya Seneti hiyo tarehe 16 Juni 2024 Karimjee Hall Jijini Dar es Salaam.

“Ndugu zangu sote hapa ni mashahidi Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alikuta kwenye mikopo ya Halmashauri kulikua na Jambo halipo sawa akisimamisha utolewaji wa Ile mikopo kwanza na Kuelekeza Watendaji wakakae waje na namna bora ya kutoa Ile mikopo ikawanufaishe walengwa”

“Sasa Ile mikopo Dkt Samia Suluhu Hassan ameirejesha ikiwa imeboreshwa, Tukumbuke kuwa Ile mikopo haina riba ni ni kwa ajili ya Vijana wote, na si ya kundi fulani fulani tu nendeni mkaombe Ile mikopo na sisi UVCCM Taifa tushatoa Maelekezo kwa Viongozi wetu huko Mikoani na Wilayani mkifika huko mtapewa ufafanuzi na maelezo ya kutosha”

Share To:

Post A Comment: