Taasisi  ya  Utafiti  wa  Wanyamapori  Tanzania (TAWIRI) ni Miongoni  mwa  Taasisi  zilizopo  chini  ya  Wizara  ya  Maliasili  na  Utalii  zinazoshiriki  maonesho  ya Karibu  KILI FAIR  2024 yanayoendelea  katika viwanja  vya  Kisongo, Magereza  Mkoani  Arusha. 


Maonyesho haya ya KARIBU KILI FAIR 2024 yamejikita  kuendelea  kukuza na kuimarisha  Utalii  ambapo mataraji ni kuyakutanisha  Makampuni 700 ya Kimataifa kutoka takribani Mataifa  50 na  Makampuni wenyeji zaidi ya 500 ikiwa ni fursa kwa Wadau  wa utalii kutangaza huduma  pamoja na kubadilishana uzoefu na makampuni mengine ya ndani na nje ya nchi. 


Aidha, Maonesho haya KARIBU KILI FAIR yameanza  katika  Viwanja  vya Kisongo- Magereza Jijini Arusha  ikiwa ni  jukwaa maalumu la kuyaweka pamoja makampuni ya ndani na nje ya nchi yanayohusika na sekta ya Utalii  na wadau wengine wa utalii. 


TAWIRI tunawakaribisha wadau kupata elimu juu ya mchango wa tafiti  za wanyamapori  katika  kukuza utalii na tunatoa ushauri wa  kitaalamu (consultancy) wa uwekezaji kwenye utalii, uanzishaji wa mashamba  ya wanyamapori (Zoo), matibabu ya wanyamapori pamoja, ufugaji bora wa nyuki na huduma mahususi ya kutoa elimu ya kisayansi  juu ya wanyamapori (Scientific  talks) 


Vilevile ,tunawakaribisha wadau kuja kuona fursa zilizopo kwenye tafiti  na namna wanaweza kushiriki na TAWIRI  ili kuwa na uhifadhi  endelevu  wa  utajiri  wa  rasilimali  ya wanyamapori  na kukuza utalii nchini


 KARIBU KILI FAIR  2024, TAWIRI tupo banda la  Maliasili  na Utalii  tembelea tukuhudumie.


Share To:

Post A Comment: