WANANCHI Mkoani Geita wametakiwa kuendelea kutumia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Mkoa huo zikiwemo za kilimo,uvuvi,ufugaji na uchimbaji wa madini ya dhahabu kwaajili ya kukuza uchumi wa Mkoa huo pamoja na wa familia zao.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingarame wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita kwenye ufungaji wa maonesho ya fahari ya Geita,ambayo yalikuwa yanafanyika kwenye viwanja wa EPZ vilivyopo Kata ya Bomba mbili Wilayani Geita.

Kingarame amesema Mkoa wa Geita umebarikiwa kuwa na fursa mbalimbali za kiuchumi hasa kwenye maeneo ya kilimo,uvuvi,uchimbaji wa madini na kwamba endapo zitatumika vizuri fursa hizi zitaweza kuleta maendeleo kwa wananchi na wawekezaji ambao wanatamani kuja kuwekeza Mkoa wa Geita.

“Katika kutambua umuhimu wa uwekezaji Mkoa wa Geita umeanzisha machinjio ya kisasa ambayo ipo Mpomvu  katika Halmashauri ya Mjini Geita hii itasaidia kuongeza ajira na kutengeneza fursa za kibiashara kwa wafugaji   na Biashara kwa wawekezaji wa ndani na nje na ndani,lakini pia Sekta ya uvuvi inaendelea kuimarika kwa kuwa na vizimba pamoja na kuwa na boti mbili za kisasa”Grace Kingarame Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Africa Creative  ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo,Raphael Siyantemi ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali  ya Mkoa kuona uwezekano wa kuweka ratiba nzuri ambayo itakuwa na utaratibu mzuri wa kupangilia maonesho hili kutokuwachanganya wadau kwani mara nyingi washiriki wanakuwa ni wale wale.



Huku Makamu wa rais wa TCCIA-Viwanda,  Boniface Ndengo,Amesema msingi mkubwa kwa sasa ambao wanao kupitia chemba ya TCCIA ni kwenda kuwasaidia wabunifu wadogo na wale ambao wanatoka mashuleni na vyuoni kuona namna ambavyo wanaweza kusaidiwa kupata masoko ambayo yatawasaidia kujitangaza na kufanya vizuri kwenye Sekta ya viwanda na ujasiriamali.



MWISHO…

Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: