1000097141


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amsema Serikali imekuwa ikijenga miundombinu mbali mbali kama vile Barabara kwa lengo la kuwasaidia Wananchi hivyo Serikali haitasita kuchua hatua kwa anayekwamisha jitihada hizo.

Mhe. Katimba amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mhe. Cosato Chumi aliyetaka kujua Je ni lini Serikali itafanya msukumo kwa Mkandarasi anayekwamisha umalizaji wa Barabara ya Kwenda kituo cha Afya Ifungu ili amalize kazi hiyo ya muda mrefu?

“miundombinu hii inayojengwa inajengwa kuhakikisha kwamba huduma za kijamii zinapatikana kwa wananchi kote Nchini, kwahiyo nimhakikishie mheshimiwa Mbunge tutaonana na kuzungumza ili tuweze kufatilia ni kitu gani kinakwamisha utekelezaji wa Miundombinu hasa katika Barabara ya Kwenda Kituo cha Afya Ifungu” Mhe Katimba.

Amesema Serikali imekuwa ikiendelea na ukarabati wa Barabara ya kutoka Kijiji cha Idete hadi Mgeta ambayo ina urefu wa Km 30.5 ambapo tayari fedha imekwisha kutengwa na Mkandarasi yupo anaendelea na ujenzi. Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Justin Lazaro Nyamoga aliyeuliza, Je lini itakamilisha ujenzi wa Barabara kutoka Kijiji cha Idete hadi Mgeta?

Aidha Mhe. Katimba amesema kipaumbele cha serikali ni kuhakikisha mawasiliano ya Barabara hayakatiki na serikali itachukua na kuiweka katika mpango wa dharura ili ili iwezekujegwa katika maeneo yeto ambayo mawasiliano ya Barabara yamekata.
Share To:

Post A Comment: