Chuo cha Uhasibu Arusha IAA kinashiriki katika maadhimisho ya Wiki ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyoanza kufanyika tangu tarehe 25-31 Mei 2024 katika viwanja vya Shule ya sekondari Popatlal, maonesho hayo yanayoongozwa na Kaulimbiu isemayo “Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi Shindani”

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano Chuo cha Uhasibu Arusha, Bi.Stella Kalinga amesema dirisha la udahili kwa ngazi ya Cheti, Stashahada pamoja na shahada ya uzamili tayari limeshafunguliwa, hivyo akawaribisha watu wenye sifa za kujiunga na katika kozi mbalimbali wajitokeze kwa wingi ili kupata elimu bora.

Bi. Kalinga amesema kuwa Chuo kinatoa elimu bora kwa kuwaandaa wanafunzi kujiajiri wenyewe lakini pia kuajiri wengine kupitia elimu ya ujasiriamali na ubunifu wanayoipata kupitia kiotamizi cha Chuo ( IAA Business Startup Center -IBSC)

“Tunawajengea wanafunzi dhana ya kujiajiri kabla hawajamaliza masomo yao Kiotamizi, hii inawasaidia wanafunzi wakifika chuoni  kuja na mawazo ya kibunifu na wanasaidiwa kuyabadili mawazo kwenda kwenye biashara halisi na kufungua kampuni".

Kupitia Kiotamizi wanafunzi wanaandaliwa kujiajiri, kuajiri vijana wenzao na kutumia bunifu zao kutatua changamoto za kijamii” Bi. Kalinga

Kwa upande wake Mratibu wa programu(IBSC), Bi. Fatma Mwanga, amesema tangu kuanza kwa mwaka wa huu wa masomo, jumla ya kampuni 10 za wanafunzi chini ya kiotamizi tayari zimesajiliwa na zinafanya kazi.

“Kwa sasa tunawanafunzi zaidi ya 190 wanaoendelea kufundishwa na kuelekezwa jinsi ya kuwa wabunifu na kwenye biashara, malengo yetu mpaka kufikia mwisho wa mwaka tunatarajia kuwa kuwa na kampuni 50 zilizosajiliwa na kuingia sokoni” Bi Fatma

Katika hatua nyingine, moja ya wanafunzi wanaolelewa chini ya IBSC, Mukhammed Costa amesema chuo kimekuwa na mchango mkubwa kuwatafutia masoko ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na wadau ili kukuza bishara zao.

Aidha, kwa niaba ya wanafunzi ametoa shukrani kwa uongozi wa Chuo kwa kuwasaidia kufika ndoto zao hata kabla ya kuhitimu masomo yao.












Share To:

Post A Comment: